PICHA: RONALDO APATA MAPOKEZI BABKUBWA NBA - LEKULE

Breaking

25 Dec 2015

PICHA: RONALDO APATA MAPOKEZI BABKUBWA NBA

Star 8
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo wa miamba ya soka ya nchini Hispania Real Madrid ametumia fursa ya mapumziko ya sikukuu za krismasi kutembelea nchini Marekani ambapo alitokea katika mechi ya mpira wa kikapu nchini humo NBA Kati ya Miami Heat na Detroit Pistons.
Star 1
Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mwanasoka tajiri zaidi hivi sasa alipokelewa kwa mapokezi mazuri huku akikabidhiwa jezi ya Miami Heat iliyokuwa imechapishwa jina lake mgongoni, sanjari na namba 7 kuonesha heshima kubwa aliyonayo staa huyo raia wa Ureno.
Star 2
Ronaldo alikabidhiwa jezi hiyo pamoja na kushiriki utani na stori pamoja na mchezaji wa kikapu wa NBA mwingereza Luol Deng ambaye alifunga points 9 katika dakika 33 alizocheza Jumanne hii na baadae kushiriki stori na Cristiano.
Star 3
Katika mechi hiyo Miami walipoteza kwa taabu kwa points 93 kwa 92 katika mchezo uliokua mkali na wakuvutia, huku mashabiki wakifurahia uwepo wa staa huyo wa soka na mshindi wa Ballon d’Or mara 3.
Star 6
Baadaye Cristiano Ronaldo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika kumshukuru Luol Deng mwingereza ambaye pia ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal, pamoja na kuishukuru klabu ya Miami kwa ukarimu wao.
Star 7
Cristiano bado yuko nchini Marekani akijipumzisha kwa ajili ya Christmas kwani bado Ana muda wa kutosha kabla ya kurudi Hispania kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu nchini humo pamoja na michuano mingine.
Star 4

Star 5

No comments: