Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa
kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka
wafanye kazi tu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha
Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu
taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.
Amesema
kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kwamba sheria na katiba ya
nchi lazima ifuatwe na watu wote nchini bila kujali cheo cha mtu
aliyetoa matamko hayo.
Masaju
amesema kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote ofisini kwake kutokana
na matamko hayo ambayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari
pekee .
Katika
mahojiano hayo,Masaju alikataa kueleza moja kwa moja kama uamuzi huo
unaochukuliwa na baadhi ya wakuu wa mkoa ni kosa kisheria.
“Mimi
sio Jaji wa kusema kuwa waliosema hivyo wamevunja sheria, lakini nataka
kusema kuwa sisi sote tunaongozwa na sheria na katiba ambavyo lazima
vifuatwe.” Alisema Masaju.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos
Makalla wametangaza kusitisha likizo kwa watumishi katika mikoa hiyo kwa
sababu za kuwataka wafanye kazi tu!
Kwa mujibu wa sheria, likizo ni haki ya mfanyakazi.
No comments:
Post a Comment