MSAFARA WA WAZIRI MUHONGO WAPATA AJALI, HAKUNA ALIYEJERUHIWA - LEKULE

Breaking

29 Dec 2015

MSAFARA WA WAZIRI MUHONGO WAPATA AJALI, HAKUNA ALIYEJERUHIWA

mug1

Msafara wa Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo umepata ajali baada ya magari mawili kuacha njia katika Kijiji cha Kagorogoro Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera.
Hata hivyo Afisa habari wa wizara hiyo Bi. Asteria Muhozya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema katika ajali hiyo hakuna majeruhi na walifanikiwa kubadilisha matairi yaliyokuwa yamepasuka kutokana na msukosuko wa kuacha njia  na kuendelea na safari,  Msafara huo ulikuwa unatoka mpaka wa Murongo karibu na nchi jirani ya Uganda.
mug2 mug3

No comments: