INTERNATIONAL
hospitality consultancy HD Partnership (HDP) kwa kushirikiana na
shirika la wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), wanafanya mkutano wa awamu
ya pili wa mwaka Disemba 7 na 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii,Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.
Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii,Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.
Mkutano
huu ambao unahusisha wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi, una lengo
la kuchochea ukuaji endelevu wa sekta hizi kwa kutoa wataalamu husika
kuongea na kutoa ushauri pia kutengeneza mazingira ya maonyesho ambayo
yatatoa fursa za kubadilishana ujuzi baina ya kampuni tofauti kwenye
sekta ya ukariimu na utalii. Kwa mujibu wa Meelis Kuuskler ambaye ni
mshauri wa kimataifa kuhusu ukarimu na Mkurugenzi mkuu wa HDP anasema “
mkutano wa mwaka huu umejikita katika masuala maalumu ya kiutendaji
yanayoathiri shughuli za kiutalii.
Ikiwa
ni pamoja na mjadala kuhusu jinsi gani ya kuiinua ubora wa rasilimali
watu, jinsi ya kuchochea zaidi mazingira mazuri ya biashara kwa
maendeleo mapya na yaliyopo ya ukarimu, na jinsi ya kuimarisha uhusiano
wa sekta zinazoingiliana kwa maendeleo endelevu ya sekta”.
Tanzania
inashika nafasi ya 7 kati ya nchi 141 kwa mwaka 2015 katika ushindani
wa sekta ya utalii kutokana na rasilimali za asili nyingi zilizopo, hii
ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jukwaa la uchumi duniani.
Hata
hivyo, ripoti pia inaeleza umuhimu wa kuboresha miundo mbinu na
mazingira ya kibiashara ili kuimarisha ushindani wa sekta hii kwa
ujumla. Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Tanzania imejaliwa kuwa na
mbunga za wanyama, fukwe na vivutio mbali mbali vinavutia uwekezaji
mkubwa katika sekta ya ukarimu na utalii.
Hata
hivyo, faida za maliasili hizi haziwezi kujulikana kwa undani zaidi
mpaka masuala kama usafiri wa anga na nchi kavu, soko la ajira and sera
za mazingira endelevu zimepatiwa ufumbuzi. Kwa mujibu wa Lathifa Sykes
Mkurugenzi mkuu wa HAT anasema “Vikwazo hivi katika maendeleo ya sekta
haviwezi kushughulikiwa ipasavyo na sekta binafsi lakini badala yake
vinahitaji ukaribu na umakini zaidi wa kiutendaji wa sekta za umma”.
Waandaaji
wa HRT mwaka huu wamebaini umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanawashirikisha
watendaji wa sekta za umma ili kupata mitazamo, mawazo na taarifa za
kutoka kwa watendaji hao ili zishirikishwe kwenye sekta binafsi. Na
mialiko imefikishwa hadi kwenye wizara ya kazi na ajira, wizara ya
maliasili na utalii, idara iliyo chini ya ofisi ya rais inayoshulika na
matokeo makubwa sasa (PDB) pamoja na sekta ya uwekezaji Tanzania (TIC).
Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Uwezo wa sekta binafsi katika kutekeleza
mabadiliko utakuwa bora kama utalindwa na ushirikishwaji wa wazi wa
sekta za umma”. Kwahiyo pamoja na kutoa jukwaa la kuchochea ushirikiano
mpya, mkutano unalenga kuendeleza na kukuza dira ya pamoja ya maendeleo
na harakati za maendeleo kati ta ya wadau wa umma na binafsi.
KUHUSU MRATIBU.
HDP
ambaye ni mshauri wa ukarimu wa kimataifa, anafanya kazi na wateja
wetu, wamiliki, wawekezaji, shughuli za ukarimu , na mashirika ya
usimamizi ili kuendesha matokeo yanayoonekana, katika kuboresha,
kuendeleza, kutoa msaada wa kifedha na kuendesha shughuli kubwa na ndogo
za ukaarimu pamoja na miradi kadhalika ya F&B.
Ikiwa
na ofisi zilizoko nchini Dubai, HDP walileta ofisi yake nchini Tanzania
mwaka 2014 ili kusaidia ukuaji mahiri na endelevu wa utalii na ukarimu
katika Afrika Mashariki. Kutumia utaalamu mkubwa wa washirika, HDP
inaangalia kiundani zaidi juu ya ufumbuzi wa viwango ili kuendeleza
mtazamo mpya na kufanya mashirika yawe ya ushindani zaidi. Kwa njia ya
uchambuzi wa hali ya juu kwa kila mteja na kuendeleza ufumbuzi wa wateja
ambao unakidhi mahitaji ya shirika husika.
KIINGILIO NI BURE KWA WAJUMBE WOTE WA TANZANIA.
Kiingilio
ni bure kwa wajumbe waliojisajili mtandaoni. Tunawahamasisha wamiliki
hoteli, mameneja, mawakala wanunuzi, wawekezaji na wadau wote kuungana
na sisi, ili muendeleze na mkuuze biashara zenu sasa.
Kujisajili tafadhali tembelea tovuti ifuatayo http://www.hospitalityroundtabletz.com/
No comments:
Post a Comment