Baadhi ya
wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu waliofika Bandari Kuu ya Zanzibar
kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikitokea Korea
kusini.
Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
Waziri
wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya
matumizi ya gharama zilizotumika mara baada ya kuwasili kwa Meli ya MV.
MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.
Meli ya MV MAPINDUZI II yatia nanga Bandari kuu ya Zanzibar ikitokea Korea Kusini.
.
Na Naryam Kidiko MAELEZO Zanzibar.
MELI
mpya ya MV.Mapinduzi ( ii) imewasili bandarini zanzibar kwa ajili ya
kuanza safari zake baada ya kukamilika ujenzi wake huko korea ya
kusini.
Hafla
ya kuwasili kwa meli hiyo imeongozwa na waziri wa fedha Omar Yussuf Mzee
ambapo amesema ujenzi wa meli hiyo ni agizo la Raisi wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Moh’d shein.
Amesema
meli hiyo bado iko katika mikono ya wajenzi hadi sasa na inatarajiwa
kuzinduliwa rasmi wiki ijayo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Moh’d Shein
ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Waziri
mzee amesema meli hiyo inavifaa vya kutosha kama vile life jacket,
pamoja na boti ndogo ili kuweka usalama kwa abiria wataosafiri katika
meli hiyo.
Hata
hivyo amesema meli hiyo itasafiri pemba pamoja na Dare-salam hivyo
amewataka wananchi kuitunza meli hiyo kwani ni matunda yao.
Nae
Katibu Mkuu Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano Zanizar Dk. Juma Malik
amesema lengo kulifanya shirika la meli lifanye kazi kibiashara ili
kuongeza pato la Taifa.
Amewaomba
wananchi kuitunza na kuitumia vizuri meli hiyo kwani wamefanya kazi
kubwa na kutumia gharama hadi kufikia kukamilika kwa meli hiyo.
Sambamba na hayo amesema meli hiyo ina uwezo wa kupakia abiria wasiopungua 1,200 pamoja na tani za mizigo 200.
Meli
hiyo mpya ya MV.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu
jumla ya dola mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika
umechukua jumla ya miezi 18.
Imetolewa na maelezo zanzibar.
No comments:
Post a Comment