MANCHESTER UNITED YAFUNGWA NA STOKE CITY 2-0 - LEKULE

Breaking

27 Dec 2015

MANCHESTER UNITED YAFUNGWA NA STOKE CITY 2-0

Kipindi cha kwanza kimemalizika 2-0 Stoke wanaongoza mpaka sasa.2-0Bojan Krkic dakika ya 19 anaipatia bao la kwanza Stoke City, Bao la pili lilifungwa na Marko Arnautovic dakika ya 26.
VIKOSI:
Manchester United XI (4-2-3-1):
De Gea; Young, Smalling, Jones, Blind; Carrick, Herrera; Mata, Fellaini, Depay; Martial.
Subs: Romero, Varela, McNair, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Pereira, Rooney.

Stoke XI (4-2-3-1): Butland; Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters; Cameron, Whelan; Shaqiri, Afellay, Arnautovic; Bojan.
Subs: Haugaard, Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Diouf, Walters.

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6 zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,
Rooney amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na tunajionea fahari kuichezea Manchester United."Leo tutakazana mkuu!

No comments: