Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery.
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya
anayefanya vizuri, Malaika Exavery amesema anakerwa na kitendo cha watu
wengi kumfananisha na muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na LEKULE, Malaika
alisema huko nyuma alipokuwa akifananishwa na msanii huyo hakujali,
lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda imekuwa ni shida hadi wengine
wanamsimamisha.
“Unajua kufananishwa na mtu siyo tatizo,
lakini kwa hali ilivyo hivi sasa lazima mtu usikie kuchoka kabisa kwa
sababu hata wakati mwingine unaendesha gari mtu anakusi mamisha halafu
akikuangalia usoni vizuri anaondoka, anasema alidhani ni Lulu,” alisema
Malaika.
No comments:
Post a Comment