Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani
akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani
ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu
kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya
moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Askari
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SGT.
Tunu Kuta(kulia) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la
kwenda mikoani, Masoud Seleman ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la
polisi kitengo hicho katikati Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa
huo SSP Nuru Selemani na wapili kulia ni Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa
Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani.
Kaimu
mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)akimpa
maelezo dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud Selemani kuhusiana na
pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi
la Polisi kitengo cha Usalama barabarani yenye ujumbe“Wait To Send”
unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo
cha mabasi yaendayo mkoani cha Dodoma.Katikati Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani.
Mkuu
wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu
ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa elimu kwa abiria ndani ya basi
liliendalo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Dodoma ikiwa ni sehemu ya
mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva
kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni
hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani(kulia)
akitoa maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)Kuhusiana na
mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva
kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni
hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.Wengine kutoka kusho ni Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na Kaimu Mkuu wa kanda ya
kati wa kampuni hiyo Heladius Kisiwani.
Baadhi
ya Madereva wa mabasi yanayosafirisha abiria mikoani wakimsikiliza
Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)
akiwapatia elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la
Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Shughuli
ikiendelea ya kutoa elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi
la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Kampeni
ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za
usalama barabarani,leo imefanyika katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva
wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia
ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms)
wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Mkuu
wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani
amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali
“Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa Dodoma ni wengi hususani madereva
wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa
tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza
ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema
madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali
zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua hususani katika kipindi hiki
cha msimu unakoelekea wa sikukuu na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa
kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo
limekuwa sugu.
Kwa
upande wake,Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa asoko wa Vodacom Tanzania
Heladius Kisiwani, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali
katika kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama
lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha
murua na marefu.”Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia sheria za
barabarani na kutokutumia simu wakati wowote wakiwa wanatumia vyombo vya
moto".
Aliongeza
kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za
kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni
ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia
sheria za usalama barabarani.
Alisema
kampuni hiyo itaendeleza kutoa elimu kwa mikoa mingine pia katika
uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya
Morogoro,Dar es Salaam na mikoa mingine na kampeni hizi zitaendelea
kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika
kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa
usalama barabarani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na
simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za
kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama
wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendesha
vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Baadhi
ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Dodoma wamesema ni ya muhimu
itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea
hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi
zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Sunday Israel
mkazi wa Dodoma aliyekuwa safarini kuelekea Singida.
No comments:
Post a Comment