Wachezaji
wa Timu ya JKU wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya KVZ kabla ya kuaza
mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar
Timu ya JKU imeshinda 2-0.
Mchezo
uliochezwa jioni mabao ya JKU yamefungwa katika kipindi cha kwanza na
katika dakika ya 8 mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande ameipatia
bao timu yake katika dakika ya nane ya mchezo huo kipindi cha kwanza na
Bao la ushindi la JKU limepatikana katika kipindi hicho cha kwanza
katika dakika ya 35 ya mchezo huo lililofungwa na mshambuliaji wake
Nassor Mattar.
Kocha Mkuu wa Timu ya KVZ King akifuatilia mchezo huo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2-0.
Beki
wa timu ya KVZ Juma Abdalla, akijiandaa kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya
JKU mwenye mpira Nassorv Mattar, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya
Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande(kulia) akimpita beki wa Timu ya KVZ Emill Wiliam
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Mbarouk Chande, akimiliki mpira huku beki wa timu ya KVZ Emill William akijiandaa kumzuiya.
Mshambuliaji
wa Timu ya JKU Mohammed Abdalla akimpiga chenga golikipa wa timu ya KVZ
Yakub Bakari. hatimai mpira huo na kutoka nje ya uwanja.
Mshambuliaji wa Timu ya KVZ Masoud Abdalla mwenye jezi ya kijani akimpita mchezaji wa timu ya JKU Mbarouk Chande.
No comments:
Post a Comment