Kaimu
Mkurugenzi wa KADCO ,Bakari Murusuri |(Katikati) kushoto kwake ni
mkurugenzi wa shughuli mama za kiwanja na huduma KADCO,Christopher
Mukoma na kulia kwake ni Meneja usalama wa Kiwanja, Justine Kisusi
walipokutana na wanahabari .
Kaimu
mkurug4e3nzi wa KADCO ,Bakari Murusuri akizung4umza na wanahabari
(hawako pichani ) kuhusu matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika uwanja
huo.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
Eneo la ndani la uwanja wa ndege wa KIA.
…………………………………………………………..
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.,
KAMPUNI
ya maendeleo ya viwanja vya ndege (KADCO) inayosimamia uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imekoa zaidi ya kiasi cha sh Bil 2
katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni thamani ya nyara za serikali na
vito vya thamani vilivyokuwa vitoroshwe kupitia uwanja huo.
Menejimenti
ya uwanja huo kupitia kitengo cha usalama kiwanjani hapo ilifanikiwa
kukamata kunasa vipande 264 vya madini ya Tanzanite vikiwa na uzito wa
kilograamu 2.04 ambavyo thamani yake inakadiriwa kufikia Bilioni 2.5.
Vingine
vilivyokamatwa uwanjani hapo vikiwa njiani kusafirishwa kuelekeaa
nchini Vietnam ni pamoja na kucha 261 ,meno 60 ya Simba ambayo yanadaiwa
kutokana na kuuawa kwa Simba 13 .
Kaimu
mkurugenzi wa KADCO,Bakari Murusuri aliiambia Globu ya jamii kuwa
Desemba 18 ,maofisa usalama uwanjani hapo walimkamata abiria mwenye
asili ya Uarabuni akiwa na pembe mbili za Twiga.
“Siku
ya Ijumaa tulimkamata abiria mwingine mwenye asili ya kiarabu,akitaka
kutorosha pembe mbili za Twiga na baada ya tukio hilo Jumamosi katika
ndege ya Ethiopian airlines walikamatwa abiria wengine raia wa kigeni
wakitaka kutorosha Pembe mbili za Impala nao walishikiliwa na
kukabidhiwa kituo cha polisi cha KIA.”alisema Murusuri.
Aliyekamatwa
akiwa na Pembe za Tiwiga ametajwa na idara ya uhamiaji kuwa ni Jasim
Mbarakke Alh-kubaisi (43) ambaye anaidaiwa kuwa ni mlinzi wa mfalme wa
nchi ya Qatar iliyopo katika falme za kiarabu. “Ukiangalia haya matukio
ndani ya wiki moja ,tumeweza kuokoa kiasicha fedha zisizopungua Bilioni
mbili za kitanzania,kama viongozi wengine katika viwanja vingine
,mipakani a taasisi nyingine ila mmoja atashuhudia serikkali yetu
inavyoweza kujiondesha kwa kodi za ndani”aliongeza Murusuri.
Alisema
katika uwanja huo kumekuwa na matukio mengi ambayo hayakuripotiwa
kwenye vyombo vya habari yakiwemo ya kukamatwa kwa watu 11 wakisafirisha
dawa za kulevya katika kipndi cha miaka miwli iliyopita. “Matukio
yamekuwa yakitokea mengi ,ndani ya miaka miwili iliyopita katika uwanja
huu tumekamata watu wasio pungua 11 wakijaribu kupitisha dawa za kulevya
na tayari wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria ikiwemo wengine
kufungwa jela.”alisema Mrusuri.
Murusuri
alisema kwa sasa katika uwanja huo kumefungwa vifaa vya kisasa ambavyo
vinahakikisha kwa hakuna mtu anaye pita uwanjani hapo na vitu ambavyo
havijaruhusiwa kisheria ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,John Magufuli.
Mapema
wiki iliyopita jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilitoa taarifa ya
kushkiliwa kwa watu wanne wakiwamo raia wanne kutoka mataifa tofauti kwa
makosa mbalimbali, akiwemo aliyekutwa na nyara za serikali kinyume cha
sheria.Kamanda wa polisi mkoani hapa, Fulgence Ngonyani alisema tukio la
kwanza lilitokea Dec 15 majira ya saa 10.00 alasiri katika uwanja wa
ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alikamatwa raia wa
Vietnam,Hoang Nghia Trung(49) akitaka kusafirisha nyara hizo.Alisema
mtuhumiwa huyo alihifadhi nyara hizo katika mabegi yake ambapo maofisa
wa usalama katika uwanja wa ndege wa KIA walimtilia shaka na kufanya
upekuzi katika mabegi yake ndipo walipokuta nyara hizo zikiwa
zimehifadhiwa ndani ya mabegi hayo.
Hata
hivyo thamani halisi ya nyara hizo bado haijajulikana na mtuhumiwa
anaendelea kuhojiwa na atafikisha mahakamani mara
upeleleziutakapokamilika.
Katika
tukio jingine ,Anurag Jain(45) raia wa India alikamatwa uwanja wa ndege
wa Kia akiwa na madini ghafi aina ya Tanzanite vipande 264 bila kibali
akiwa amehifadhi kwenye mabegi yake akielelekea Hong Kong China.
No comments:
Post a Comment