Elizabeth
J. Kisamba, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama ya Wilaya Temeke Dar
es Salaam, akichangia mada katika mafunzo ya Huduma kwa wateja,
yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Praxeda
S. Joseph, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama Kuu Tabora, akifafanua
jambo juu ya mada iliyotolewa katika kuboresha huduma kwa wateja
mahakamani.
Watumishi
wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya
Huduma kwa wateja ili kuweza kuwajengea ujuzi na ufanisi katika kazi
mahakamani.
Simon
Berege, Mwenyekiti wa MISA-TAN Afrika, akielezea umuhimu wa mafunzo ya
huduma kwa wateja hasa kwa watumishi wa Mahakama ili kuweza kutoa
taarifa sahihi ambazo zitarahisisha kutoa haki na kwa wakati.
Bw.
Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, akitoa
risala fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya Huduma
kwa Wateja kwa Watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
Mhe.
Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, akifungua rasmi
mafunzo maalumu ya Huduma kwa Wateja kwa watumishi wa Mahakama ya
Tanzania, leo mkoani Dodoma.
Mhe.
Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, (aliyeketi wa
pili toka kushoto), Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama
ya Tanzania, (wa pili kulia), Deus Kibamba, Mkurugenzi wa TCIB, (wa
kwanza kulia), Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, (wa kwanza
kushoto), katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kada mbalimbali wa
Mahakama ya Tanzania washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Wateja,
Mkoani Dodoma.
MAFUNZO
maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata
taarifa kwa watumishi wa Mahakama, yamemalizika leo katika hoteli ya
St.Gaspar mjini Dodoma.
Akifungua
rasmi mafunzo hayo Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mhe. Crescencia
Makuru, amesema moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo, ni kuwajengea
uwezo watumishi wa Mahakama kwa kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali
itakayowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
“Mahakama
ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama
sehemu ya kuhakikisha kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati”,
Jaji Makuru amebainisha.
Mwaka
2014 Mahakama ya Tanzania kama moja ya Taasisi ya Serikali ilifanyiwa
tathmini kuhusu utoaji wa haduma zake hasa katika nyanja ya upatikani na
utoaji wa taarifa kwa Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini mwa Afrika, (Media Institute of Southern Africa-MISA).
Katika
tathmini ile, Mahakama ilikuwa ya mwisho na ilizawadiwa kufuli la
dhahabu kama alama ya kuonyesha kuwa taasisi hii ni moja kati ya
zilizojifunga sana kutoa taarifa kwa wananchi. Moja ya maeneo
yaliyoonekana na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea na
kutunza nyaraka na hata wanavyowahudumia wateja kwa ujumla.
Mafunzo
hayo endelevu yamelenga kuwafundisha makarani na watumishi wa kada
mbalimbali nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini?, Huduma kwa
wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa Umma , Njia mbalimbali
za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za Umma na Sheria ya utoaji wa
habari katika Mahakama.
Mafunzo
haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa
kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA)
pamoja na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment