Hii Ni Sawa Kabisa; Anayeota Kuwa Meya Wa Jiji Asifikirie Anaweza Kununua Na Ufukwe Wake Pia.. - LEKULE

Breaking

9 Dec 2015

Hii Ni Sawa Kabisa; Anayeota Kuwa Meya Wa Jiji Asifikirie Anaweza Kununua Na Ufukwe Wake Pia..



Ndugu zangu,

Meya wa Jiji Dar hata nyumba yake inapendeza zaidi akizungushia makuti, badala ya ukuta. Iweje leo anayeota kuwa meya wa Jiji la Dar es Salaam anafikiria hata kuwawekea ' ukuta' watu wake.
Kumiliki ufukwe ina maana ya wanyonge wengi kukosa fursa ya kwenda kuvinjari bila kulipia. Meya anapaswa kufikiria kupanda miche ya minazi zaidi kando ya ufukwe ili watu wake wapate mandhari nzuri zaidi.
Siku zote nitakuwa mtu wa mwisho kukubali fukwe zetu aina ya Coco Beach zitwaliwe na wachache. Nitakuwa ni mmoja wa watakaopiga kelele.

No comments: