Mwanasiasa mkongwe nchini, Juma Duni Haji amesema hatima yake ya kubakia au kuondoka ndani ya Chadema itajulikana mwezi ujao.
Duni
aliihama CUF na kujiunga Chadema ambayo ilimsimamisha kuwa mgombea
mwenza wa urais wa Chadema iliyokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NLD na NCCR Mageuzi.
Tangu
kuisha kwa Uchaguzi Mkuu na mgombea wa Chadema kushika nafasi ya pili,
Duni amekuwa kimya, lakini juzi alisema itakapofika Januari mwakani
ataeleza mustakabali wake kisiasa.
“Kwa
sasa sisemi jambo lolote, nitakuambia baadaye kidogo kama nitarudi CUF
au nitabakia Chadema. Kuna mambo ninafanya kwanza, nisingependa kusema,”
alisema Duni.
Pia,
Duni alizungumzia hisia zake za kisiasa visiwani Zanzibar, akisema
anashangazwa na kauli ya aliyekuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Mark Bomani kumshawishi Maalim Seif Hamad akubali
uchaguzi urudiwe.
Siku
chache zilizopita, Jaji Boman alinukuliwa na vyombo vya habari akimtaka
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kukubali kurudia uchaguzi huo kama ilivyotangazwa na
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kuwa
utarudiwa ndani ya siku 90.
Jecha
alifuta matokeo ya urais na uwakilishi wa Zanzibar, akisema kulikuwa na
ukiukwaji wa sheria na kanuni na kwamba ndani ya tume yake wajumbe
walitofautiana hadi kukunjana.
Jaji Bomani alisema kama Maalim Seif alishinda, atashinda uchaguzi ukirudiwa kwani wananchi watampigia kura.
Hata
hivyo, Duni alisema: “Anajua kabisa nchi yoyote inaporudia uchaguzi
mara nyingi amani huwa inapotea, kwa mfano Burundi leo hii bado wanauana
na hakuna anayezungumza lolote kwa sababu ni chama tawala kimeshinda.
“CUF
inasisitiza Katiba ya Zanzibar ilindwe au kwa sababu upande wa Bara
wamepata Rais (John Magufuli), sasa hawajali usalama wa Wazanzibari?”
Duni
alihamia Chadema chini ya mpango maalumu wa Ukawa wa kuwezesha vyama
hivyo kuchukua urais Bara na Visiwani, mpango ambao haukuweza kuzaa
matunda.
No comments:
Post a Comment