Wakati
joto la kusubiri rais John Magufuli atangaze majina ya baraza lake la
mawaziri likizidi kupanda, gazeti la Mwanahalisi limetoa baadhi ya
majina yanayodaiwa kuvuja kutoka kwenye orodha hiyo.
Mmoja
kati ya majina ambayo yamevuta usikivu wa wengi ni jina la aliyekuwa
waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe ambaye alikuwa mmoja kati ya
wagombea wa CCM waliokuwa wanatajwa kuwa chaguo la rais mstaafu, Jakaya
Kikwete.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwana Halisi, majina mengine yanayotajwa ni pamoja na January Makamba,Dk. Asha Rose Migiro,Ridhiwani Kikwete,Peter Serukamba na Mwigulu Nchemba.
Jina
jingine lililotajwa kwenye orodha hiyo ni jina la aliyekuwa Makamo Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Dk. Charles Kitima.
Dk.
Kitima anadaiwa kuwa mmoja kati ya watu waliomuamini sana Dk. Magufuli
wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na hata kumualika kuwa mgeni rasmi kwenye
mahafari ya chuo hicho.
NB: Majina haya ni kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi ambalo limedai kuyapata baada ya kuvuja. Rais Bado hajatangaza baraza lake la mawaziri
Hata hivyo,Rais Magufuli anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri muda wowote kuanzia sasa.
Kwa mujibu wa katiba, rais anapaswa kutangaza baraza lake kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge vya mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment