Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
“Nadhani
sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa
Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo
inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi
sana,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema.
Amesema
kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili
usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika
hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
No comments:
Post a Comment