Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo majira ya jioni amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho.
Mara
baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi
mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna
daktari aliyekuwa anatoa huduma.
Akizungumza
na wagonjwa waliokuwa wakisubria tiba alisema kuna waliofika katika
kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia
wagonjwa hao.
Katika
ziara hiyo ya kushtukiza ambayo Dr Mwaka na wasaidizi wake walikimbia,
msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema
lolote kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu,hivyo alimwomba
Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwauliza
maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya kituo hicho.
Baada
ya ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi
Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya
ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika
kuhusu taaluma ya Dr. Mwaka pamoja na washirika wake na pia dawa
anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dawa hizo.
Pia amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini jambo ambalo ni kosa kisheria.
Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika mojawapo ni kutojitangaza.
Naibu
waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na
amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile amesomea udakitari wakati
sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tiba Asilia na
Tiba Mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.
Pia
Naibu Waziri amemtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa
mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya
Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia
kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.
No comments:
Post a Comment