Denti chupuchupu kubakwa ufukweni - LEKULE

Breaking

30 Dec 2015

Denti chupuchupu kubakwa ufukweni



IMG_1317
Maria akisitilia na marafiki zake baada ya kunusurika kubakwa.
Deogratius Mongela na Chande Abdallah
SIKUKUU NOMA! Zikiwa zimepita siku chache baada ya Sikukuu ya Krismasi kupita, imeacha matukio ya hatari ambapo denti wa Shule ya Zanaki, Dar aliyejulikana kwa jina moja la Maria alinusurika kubakwa katika Ufukwe wa Coco Beach.
Tukio hilo lilinaswa na kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), siku ya ‘Boxing day’ ambapo denti huyo alinusurika kubakwa na wanaume wakware waliokuwa wakimzengea zengea wakati alipokuwa akibadilisha nguo baada ya kutoka kuogelea.
IMG_1306Inadaiwa kuwa Maria alifika Coco Beach majira ya saa 7 mchana akiwa na marafiki zake wawili wa kiume na kubadilisha nguo katika moja ya vichaka vilivyopo eneo hilo na kuingia baharini huku nguo zake akimkabidhi mmoja wa marafiki zake hao.
Baada ya kumaliza kuogelea, Maria alichukua baadhi ya nguo zake na kwenda kubadilisha ndipo alipovamiwa na wanaume hao wasiojulikana na kutaka kumfanyia ufuska huo ambapo alipiga kelele zilizosababisha marafiki zake kwenda kumuokoa huku wanaume hao wakitoka nduki.
IMG_1320
….Wakimpeleka sehemu salama.
Mara baada ya kunusurika kufanyiwa kitu mbaya msichana huyo na marafiki zake hao waliamua kuondoka eneo hilo na kurudi nyumbani kwa hofu ya kitendo hicho.

No comments: