Chama cha Wananchi (CUF) kimekanusha vikali taarifa zilizosambazwa na watu ambao hawajajulikana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki.
Akiongea
na ITV, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano na Umma wa chama
hicho, Ismail Jusa amesema kuwa taarifa hizo zina lengo la kuvuruga
amani na usalama wa nchi kwa kutengeneza taharuki.
Jusa
ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa waliopika
na kusambaza habari hizo kwa kuwa mbali na kuwa kiongozi wa chama na
mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif ni Kiongozi wa ngazi za juu wa
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar..
“Yeyote
aliyekuwa nyuma ya kusambaza uvumi huu hakuwa na nia njema. Na utaona
kama ina malengo ya kisiasa kwa sababu taarifa yenyewe imehusishwa
kwamba eti tukio hilo limetokea baada ya kujaribu kuwashawishi wajumbe
wa vikao vyake vya CUF eti wasaini waraka wa kutaka uchaguzi urudiwe,
jambo ambalo halipo,” alisema Jusa.
Taarifa
hizo za kugushi zilizosambaa ziliwekewa nembo ya mtandao wa Facebook wa
ITV, hali iliyokilazimu kituo cha ITV kukanusha vikali kuhusika na
taarifa hiyo.
Katika
hatua nyingine, Jusa alieleza kuwa msimamo wa CUF kuhusu uchaguzi wa
Zanzibar uko wazi kuwa hakuna kurudia uchaguzi na kwamba mshindi ambaye
wanaamini ni Maalim Seif atangazwe
No comments:
Post a Comment