Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo kwa mawaziri hao.
Nia
ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata
mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na
wawajibikaji.
Chanzo
cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaeleza
kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake kutokana
na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya
kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali
uteuzi huo.
Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa ya mkataba huo.
“Kwa
sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri na
Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote
atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.
“Mikataba
ya Mawaziri na Manaibu inalenga kuwabana watumishi hao na kukubaliana
kuwa iwapo itatokea tatizo katika wizara husika wao watakuwa wa kwanza
kuwajibishwa.
“Mkataba
unalenga kuwafanya Mawaziri hao na Manaibu wao kuhakikisha wanafanya
kazi kwa uaminifu, uadilifu, na kwa kujali maslahi ya jamii,” kilisema chanzo hicho.
Pia
kilisema mkataba huo unaonekana unamasharti kwamba endapo siku mawaziri
hao watajiingiza kwenye vitendo vya kifisadi au Wizara husika kulaumiwa
watalazimika kujiuzulu bila kubembelezwa huku mhusika akifishwa kwenye
vyombo vya sheria bila mjadala.
Aidha,
chanzo hicho kiliongeza kuwa kwa sasa wabunge waliowengi wanaogopa
nafasi za uwaziri na unaibu kwa madai kuwa kasi ya Rais Magufuli ni
kubwa na inaweza kumtia hatiani mtumishi wakati wowote.
“Wabunge
hao wanapata homa kubwa kutokana na hatua ya Rais Magufuli na Waziri
Mkuu Majaliwa kuonesha ushujaa wa ajabu kwa kuwashambulia vigogo ambao
wameshindikana katika vitendo vya ukwepa wa ulipaji kodi au kufanya
ubadhilifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandari.
“Kitendo
kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo Kikwete (Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana inaonesha
wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi basi
kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.
“Sikiliza
kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara wakubwa na matajiri
wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama kutokujua
anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu wanayotoa
katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo waliyonacho na
wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.
Wakati
huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais Magufuli kwa sasa
ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha katiba ya
chama hicho.
Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.
“Hofu
hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana akiwa mwenyekiti
watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa na wakati
mgumu zaidi.
“Mbali
na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa wanapatiwa madaraka
kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani waliowengi wanaweza
kutimliwa,” kilisema chanzo hicho.
No comments:
Post a Comment