Mashambulizi ya mjini California yaligharimu maisha ya watu 14
Rafiki wa
wapenzi waliotekeleza mashambulizi na kusababisha mauaji ya watu 14
mjini San Bernadino huko califonia nchini Marekani mwanzoni mwa mwezi
huu amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kushirikiana kufanya kosa la
ugaidi.
Enriquez
Marquez anashutumiwa kununua silaha mbili kinyume cha sheria ambazo
zilitumika na Syed Rizwan Farok na Mkewe Tashfeen Malik pia alinunua
malighafi iliyotumika kutengeneza Bomu.
Marquez amekana mashtaka akisema kuwa hakufahamu mipango ya wapenzi hao.
Mtu
mwingine Jalil bin Ameer Aziz amekamatwa pennyslvania kwa kosa la
kushiriki na kujaribu kutoa msaada wa mali kwa kundi la Islamic state
wapelelezi wanasema Enriquez alibadili dini na kuwa muislamu baada ya kufahamiana na jirani yake Syed Rizwan Farook.
Inaelezwa
kuwa walikuwa wakitazama picha za video zinazohusiana na maswala ya
itikadi kali za kiislamu na walipanga mipango ya mashambulizi ya kigaidi
mwaka 2011 na 2012 huko califonia.
Maafisa
upelelezi wanasema kuwa wapenzi walipanga kurusha mabomu katika mgahawa
wa wanafunzi kabla ya kufanya mashambulizi kwa risasi . Pia walipanga
mipango ya kushambulia abiria wakiwa kwenye magari wakati wa muda wa
pilika nyingi.
Enriquez
mwenye umri wa miaka 24 anatuhumiwa pia kwa udanganyifu kuingia kwenye
ndoa ya udanganyifu na mmoja wa mwanafamilia wa Farook.kwa makosa matatu
yanayomkabili iwapo atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha jumla ya
miaka 35 gerezani.BBC
No comments:
Post a Comment