Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi
Liberata Mulamula akiwa kwenye ukumbi wa Sanaa, Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi
Liberata Mulamula akipata maelezo ya Michoro ya Mapangoni kutokwa kwa
Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi Agnes
Gidna.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi
Liberata Mulamula akipata maelezo ya Chimbuko la mwanadamu kutokwa kwa
Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Amandus
Kweka. Fuvu lilipo kulia kwenye sanduku lililo nakshiwa na dhahabu ni la
Zinjanthropus lililo gunduliwa zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyo pita
huko Ngorongoro Oldvuvai kwenye miaka ya 1959.
Balozi
Mulamula akiagana na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw
Achiles Bufure baada ya kumaliza kuitembelea Makumbushi hiyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi
Liberata Mulamula akitembezwa kujionea miundombinu ya Makumbusho na
Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo
Bw Achiles Bufure.
Na Sixmund J. Begashe
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeridhishwa na huduma
mbali mbali zinazo tolewa na Makumbusho ya Taifa kwa wageni mbali mbali
wanao tembelea Makumbusho hizo ili kujionea na kujifunza mambo mbali
mbali yanayo huyu Tanzania.
Akiwa
kwenye ziara ya kimafunzo katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar
es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Balozi Liberata Mukamula amesema kuna umuhimu mkubwa wa
kuitumia Makumbusho za Taifa ili kutoa elimu kwa wageni mbali mbali
wanaotembelea Tanzania.
Ameongeza
kuwa Wizara yake hupokea wageni wengi wa kimataifa wanaokuja kwa
shughui za kiserikali hivyo ofisi yake itafanya utaratibu wa kuhakikisha
wageni hao wanatembelea makumbusho kwa maana ndio sehemu pekee wanapo
weza kuifahamu Tanzania kwa muda mfupi bila kuizunguka nchi yote.
“Nimekuja
mwenye kujionea na kujifunza huduma mnazo toa hapa, ili nijiridhishe
kwanza kabla ofisi yangu haijaanza kuwaleta wageni hapa, kiukweli
nimeridhishwa sana na huduma yenu na licha ya kujifunza nimeona vipo
vivutio vingi vinaweza kuwavutia wageni wa kiserikali na kujifunza
kupitia vitu hivi, hongereni sana” Alisema Balozi Mulamula.
Akimshukuru
Balozi Mulamula kwa kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure
alisema kuwa amependezwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuona umuhimu wa
kuitumia Makumbusho kama Mwalimu Mwelekelezi wa Mambo yanayo thaminiwa
na watanzania
“Viongozi
wetu wa kubwa wakienda kikazi nchi za wenzetu, wakifika huko hutembezwa
Makumbusho, ili kuwafanya wasiondoke bila kuzifahamu hizo nchi
kihistoria na hata kimaendeleo ya kisayansi na teknolojia, vivyo hivyo
wanapokuja hapa nchini wanapaswa kutembezwa Makumbusho ili wapate sura
sahihi ya nchi yetu” Aliongeza Bw Bufure.
Mkurugenzi
huyo wa Makumbusho ametoa wito kwa Wizara zote za Serikali, Taasisi za
watu binafsi na Watanzania kwa ujumla wenye kutembelewa na wageni
kutoka nje ya Tanzania kuwa na Utamaduni wa kuwatembeza wageni wao
Makumbusho ili kujifunza mambo ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment