Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alipotembelea
kwa mara ya kwanza Wizara ya Fedha, safari ambayo ilikuwa ni ya ghafla.
[TANZANIA]
Kwa sasa kila zungumzo la Mtanzania ni juu ya safari za kushtukiza za
Rais wa awamu ya tano, Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameacha
gumzo kwa kuanza kwa kishindo na dhana yake ya ‘Hapa Kazi Tu’!.. Kwa
kutuonjesha tu, ametembelea Wizara ya Fedha safari ya kushtukiza na
kuamsha hali ya utendaji wa kazi kwa watumishi wa idara ndani ya Wizara
hiyo ambapo baadhi yao hawakuwapo kwenye viti vyao kwa kile
kilichoelezwa kuwa wameenda kupata chochote kitu! (Hatushangai hilo
kwani tumbo nalo linahitaji kupata chochote kitu).
Dk.
Mafuguli amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya taifa
Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa lakini hali
aliyokutana nayo nadhani majibu yake kila mmoja anafahamu na hata sasa
moja ya mashine ya kupima magonjwa makubwa inafanya kazi huku
tukishuhudia Afisa habari wa idara hiyo akikadhana kutoa taarifa kwa
vyombo vya habari kuwa kifaa hicho kimeanza kufanya kazi na vifaa
vingine vinaendelea kushughulikiwa. (Tunapongeza kwa hilo ila tunasema
kuwa Watanzania tuache kufanya kazi kwa mazoea tena mazoea ambayo
yametuumiza kwa muda mrefu).
Kwa
kuona umuhimu tu wa kipekee ili kufanya kazi pasipo kufuatwafuatwa ni
wakati sasa Watanzania tupige kazi kwa nguvi zote kusaidia Taifa kusonga
mbele.
Rais
Dk. Magufuli tunaomba pia utembelee na huku…!!! najua kila mtu
atajiuliza na ‘Huku’ kuna Idara nyingi tu za Serikali zimekuwa
zikishindwa kufanya kazi zake ipasavyo kisa wao ndio kila kitu katika
Taifa hili?, Sasa Rais kama utapata muda unaweza ‘kuibuka’ kama
wanavyosema lugha ya vijana ama kutokea ghafla hapo tu hatua chache
kutoka Ikulu yetu tukufu yaani kuibukia kwa Wazee wa Bandari, yaani huku
Bandarini kila mtu ni mtemi licha ya kila awamu ya uongozi kupafanyia
marekebisho mahala hapo lakini mizizi yake ni mipana mno jicho la wengi
ni nani ataangusha ‘mbuyu’ bandarini?.. tembelea hapo kuna madudu mengi.
Pia
Rais wetu Dk. Magufuli tembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) huku nako kuna
tuvituvitu twingi sana kama utapata muda wewe fanya kama unapita tena
unaweza kwenda hata saa 10 jioni ama saa sita mchana maana napo
wamejisahau sana licha ya hapa kuwakumbusha najua hawata fumbua masikio
yao.
Pia
chungulia huku kwa taasisi ya Rushwa TAKUKURU nako sijui kama
wamesadiki na kasi yako maana kupo kaa hakupo vile fanya kama unaenda
kunywa nao chai na kujionea tuvituvitu na huenda wasiwe na hata ripoti
kamili za wahusika ila watakupatia makabrasha ya watu wanaowafuatilia
miaka nenda rudi.
Kama
utaweza Mkuu wetu Dk. Magufuli angazia huku uwanja wa ndege wa Mwalimu
Nyerere JNIA maana nao una tuvituvitu sasa fanya kama unaenda safari ya
mbali kumbe ndio unaenda kuona utendaji wao wa kazi naona nao kama
wamejisahau vile maana ukiwauliza madereva teksi watakuambia pale bana
pamopamo tu!!
Tunajua
huku kuko kwingi ila tunakuomba pia unaweza kuwatembelea TFF maana nao
wanashindwa kuisogeza mbele Taifa Stars endapo utapitia pale basi
utakuwa kama umewatingisha nadhani hata Taifa Stars inaweza kuifunga
Algeria katika mchezo wake wa kufuzu kombe la Dunia.. achaa nimalize na
hapa kwanza Ila watanzania tuache kufanya kazi kwa mazoea.
No comments:
Post a Comment