Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia)
akimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Mhandisi Kapuulya
Musomba (katikati). Wa Kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi
Paul Masanja.
Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba
Baadhi ya mitambo kwenye Kituo cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) na
Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja mara baada ya kukagua Kituo cha
Kuchakata Gesi asilia cha Madimba.
Wataalamu
wa Kitanzania wanaofanya kazi kweye Mradi Mkubwa wa Gesi Asilia nchini
wametakiwa kuhakikisha wanajifunza kwa ukamilifu shughuli zote za mradi
huo kabla mkandarasi hajaondoka.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,
Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja walipofanya
ziara kwenye mradi huo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi pamoja na
kuzungumza na wafanyakazi wa mradi huo.
Mbali na hilo, wafanyakazi hao walielezwa umuhimu wa kutanguliza uzalendo mbele katika shughuli zao ili kuleta tija.
Mhandisi
Chambo aliwataka wafanyakazi hao kutobweteka na badala yake wawe makini
kujifunza masuala yote yanayohusu mradi huo ili pale mkandarasi
anapomaliza muda wake waweze kueendesha wao wenyewe bila kukwama.
“Itafika
wakati lazima Mkandarasi ataondoka hivyo kama mtashindwa kujifunza
kipindi hiki itawapa shida siku za usoni, kwahiyo hakikisheni mnajifunza
kila anachokifanya,” aliagiza Mhandisi Chambo.
Kwa
upande wake Mhandisi Masanja aliwataka viongozi wa mradi huo kuandaa
utaratibu wa kuweka wazi kazi zinazofanywa na mkandarasi ili kila
mfanyakazi aelewe nini kinafanyika bila kuwepo na kizuizi cha aina
yoyote.
“Kusiwepo
na kizuizi chochote cha nyinyi kuelewa shughuli zinazofanywa na
Mkandarasi. Pale ambapo mnafikiri bado vijana hawajaiva vizuri
hakikisheni mkandarasi anawaelekeza.
Vilevile
aliwaagiza kuboresha mazingira ya kazi na pia kuandaa utaratibu
utakaovutia vijana hao wa Kitanzania kuendelea kulitumikia Taifa lao
kupitia mradi huo wa Kitaifa.
“Mtazame
namna ambayo itawavutia wataalamu wetu waendelee kufanya kazi bila
kufikiria kuondoka; mnaweza wapa mafunzo hao ukashangaa wanahama na
hivyo kusababisha kudorora kwa baadhi ya shughuli,” alisema.
Naye
Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba
alieleza utaratibu unaotumiwa na wafanyakazi hao katika kujifunza
shughuli mbalimbali za mradi.
Alisema
wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mkandarasi kwa lengo la kuelewa
shughuli zinazofanyika ikiwa ni pamoja na matengenezo na uendeshaji wa
mitambo.
“Tupo
nao kwa ukaribu sana; wanatueleza nini watatufundisha na kwa muda gani.
Tunawauliza maswali, tunatazama namna wanavyoendesha shughuli za hapa;
hivyo nina imani muda wao wa kuondoka ukifika vijana wetu watakuwa
wameiva vya kutosha kuweza kusimamia mradi huu,” alisema.
Lengo
kuu la ziara hiyo ilielezwa kuwa ni kujionea shughuli zinazoendelea
kwenye mradi huo mkubwa wa Kitaifa wa gesi asilia pamoja na kuzungumza
na wafanyakazi wa mradi huo.
Maeneo
ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokelea
Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas
Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya
Gesi Asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu iliyoathiriwa na
Mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha
Madimba cha mkoani Mtwara.
Wengine
walioongozana na viongozi hao katika ziara hiyo ni Kamishna wa Nishati,
Mhandisi Hosea Mbise, Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi
Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia
(GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati
na Madini.
Ziara
hiyo ni ya kwanza kwa viongozi wao tangu wameteuliwa na huku ilielezwa
kwamba ni miongoni mwa mikakati waliojiwekea ya kutembelea na kukagua
miradi iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake na
vilevile kuzungumza na wafanyakazi wa miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment