Mkurugenzi
Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga
Maluleke akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya
mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika
ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu
pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu.
Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip
iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na
waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha
watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo
wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala
ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika
hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa
makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora
katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji
wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika
hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
VIONGOZI
wa Ofisi za Takwimu barani Afrika leo wamekutana kujadili Mfumo wa
Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya
Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.
Wakizungumza
katika mkutano wa wataalam wa takwimu ulioanza leo Jijini Dar es
Salaam, viongozi hao wamesema ili takwimu bora zipatikane kwa wakati, ni
lazima kuwepo na mfumo bora wa uongozi pamoja na wataalamu waliobobea
katika fani ya takwimu.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt.
Albina Chuwa amesema lengo la mkutano huo ni kujadili mfumo wa uongozi
bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na namna ya kuboresha mitaala ya
ufundishaji wa masomo ya takwimu barani Afrika.
“Leo
tupo hapa wataalamu wa takwimu kutoka zaidi ya mataifa 25 barani Afrika
ili kujadili namna ya kuboresha mifumo yetu ya uongozi katika Ofisi za
Takwimu pamoja na kujadili mbinu bora za kuimarisha utoaji wa mafunzo
kwa watakwimu vijana hasa kupitia upya mitaala ya ufundishaji,” amesema
Dkt. Chuwa.
Dkt.
Chuwa amesema kuimarishwa kwa mfumo wa uongozi pamoja na kuboresha
mafunzo kwa wakwimu kutasaidia katika ukusanyaji wa takwimu bora
zitakazotumika katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wa
Afrika ya Kusini, Risega Maluleke amesema mataifa mengi ya Afrika
yanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uwezo wa kujitegemea
kifedha kitu ambacho hukwamisha upatikanaji wa takwimu kwa wakati.
Amesema
licha ya changamoto hiyo, kwa kiasi kikubwa kazi ya ukusanyaji wa
takwimu imekuwa ikifanyika kwa ufanisi mkubwa kutoka kwa watalaam hao wa
takwimu na hivyo kupitia mkutano huu, wataweza kujadili namna ya
kuboresha uimarishaji wa Ofisi za Takwimu.
Maluleke
amesema ni vyema Serikali zikaziwezesha ofisi za ukusanyaji wa takwimu
ili ziweze kujitegemea kibajeti na kuboresha utendaji kazi wake katika
kuhakikisha takwimu bora zinapatikana kwa wakati muafaka.
Mkutano
huo wa siku tano unatarajia kumalizika tarehe 06 Novemba, 2015 ambapo
wataalam takribani 30 wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika
Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya
Takwimu katika nchi za Afrika.
No comments:
Post a Comment