Wakati Serikali ikihaha kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake, wabunge wameingia kwenye mvutano na ofisi ya Bunge kuhusu fedha ambazo wanastahili kupewa kwa ajili ya kununulia magari yao.
Mwaka
2010, wabunge walilipwa Sh90 milioni kwa ajili ya ununuzi wa magari
hayo aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop), ambayo ni vitendea kazi
vyao. Wabunge hutakiwa kulipa nusu ya fedha hizo wkati nyingine ni
mchango wa Serikali.
Lakini
wakati gharama za maisha zikipanda huku thamani ya Shilingi ikiporomoka
kulinganisha na Dola ya Marekani na hivyo kusababisha bidhaa kupanda
bei, wabunge wamekataa kulipwa kiasi hicho cha fedha mwaka huu na badala
yake wanataka walipwe kulingana na bei ya sokoni ya magari aina hiyo.
Wabunge
wanataka walipwe Sh130 milioni ambazo wanasema ni bei ya magari hayo
kwa sasa baada ya kupanda bei. Hata hivyo ombi hilo limegonga mwamba
Wakizungumza
kwa sharti la kutotajwa majina, baadhi ya wabunge walisema mara baada
ya kujisajili bungeni kwa ajili ya uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja,
katibu wa chombo hicho, Dk Thomas Kashililah alifanya kikao na wabunge
wote ili kuwapa taratibu lakini pia kuwafahamisha stahili wanazopaswa
kupata kama wabunge.
“Katibu alitujulisha kuwa hakuna ongezeko lolote la posho, hivyo tunapaswa kulipwa kiasi kilekile cha Sh300,000 kwa siku .
"Lakini pia alisema tutapewa Sh90 milioni kwa ajili ya mkopo wa gari badala ya milioni 120 ,” alisema mmoja wa wabunge hao.
"Lakini pia alisema tutapewa Sh90 milioni kwa ajili ya mkopo wa gari badala ya milioni 120 ,” alisema mmoja wa wabunge hao.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, suala hilo liliibua mjadala na kusababisha
wabunge kuhoji iweje kiwango hicho kitumike katika Bunge la Kumi na
Moja, miaka mitano baada ya wabunge wa Bunge la 10 kupewa kiasi hicho.
“Unajua
magari tunayotakiwa kununua ni Toyota Land Cruiser Hardtop, na ukweli
sasa thamani ya magari hayo imepanda sana huwezi kuifananisha na mwaka
2010 wakati wa Bunge la 10,” alisema mbunge mmoja.
Wabunge hao walitaka walipwe kiasi cha Sh130 milioni kwa madai kuwa ndiyo bei ya sokoni ya magari aina hiyo.
Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Anatropia Theonest amesema hawajakataa fedha hizo, lakini thamani ya Dola imepanda hivyo kusababisha thamani ya magari hayo kupanda pia.
“Hakuna
asiyejua kwamba thamani ya Dola imepanda na kwa kawaida kila Bunge
kunakuwa na ongezeko la Sh30 milioni. Mfano Bunge la Tisa walipewa
Sh60milioni la 10 wakapewa Sh90milioni, hivyo ilipaswa sasa iwe Sh
120mililioni ili kuendana na soko,” alisema mbunge huyo.
Akizungumzia
sakata hilo,naibu katibu wa Bunge, John Joel alisema jukumu la ununuzi
wa magari ya wabunge, lipo chini ya Serikali na siyo ofisi yake hivyo ni
bora wangeulizwa wenye jukumu hilo.
“Tunachofamu sisi mbunge anatakiwa apewe vitendea kazi likiwemo gari, lakini wanaohusika na hilo ni Serikali,” alisema.
Alisema
ofisi ya Bunge hushauriana na Serikali namna ya kutoa huduma kwa
wabunge na kwamba kwa jinsi anavyofahamu, mpaka jana watunga sheria hao
walikuwa hawajapewa fedha yoyote ya kununua magari kwa awamu hii, hivyo
wanasubiri utaratibu.
Wakati
Joel akisema Serikali ndiyo inahusika, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue aliurudisha mpira kwenye ofisi hiyo ya Bunge, akisema
uongozi wa bunge umekwisha pewa maelekezo yote na serikali juu ya ununuzi wa magari hayo, hivyo akamtaka mwandishi akawaulize wao ( uongozi wa bunge)
Katika
kukusanya fedha za kuwezesha kutekeleza mipango ya Serikali na ahadi
alizotoa wakati wa kampeni, Rais John Maguguli alitangaza hatua
mbalimbali za kudhibiti matumizi, na akawaeleza wabunge mwishoni mwa
wiki kuwa hataweza kufanikiwa iwapo hatapata ushirikiano wao.
Katika
kuonyesha kuwa anatoa kauli thabiti, Dk Magufuli aliagiza fedha ambazo
zilichangwa na taasisi mbalimbali za fedha kwa ajili ya hafla za
kuwapongeza wabunge, zielekezwe kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwenye
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Tayari
Rais ameshafuta safari za nje isipokuwa kwa kibali cha Ikulu baada ya
mtu anayetaka kusafiri kutimiza masharti kadhaa, likiwamo linalomtaka
aeleze faida ya safari yake na kama iwapo hatasafiri, nchi itaathirika
vipi.
No comments:
Post a Comment