Shirika
la Hifadhi za Taifa limezindua program maalum ambapo tembo 30
wanaoongoza makundi 30 katika mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa
watavalishwa kola malum shingoni zenye vifaa vinavyorekodi mienendo yao
kwa kutumia satelaiti. Program hii inafadhiliwa kwa pamoja na taasisi za
Global Environment Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP).
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa program hiyo hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA Allan Kijazi alisema kuwa “ Lengo kuu la program hii ni kupata
taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa
Ruaha Rungwa zitakazosaidia kubainisha maeneo ya shoroba na mitawanyiko
kwa ajili ya ulinzi wa tembo”
UNDP
kupitia ushirika wake na TANAPA/SPANEST wametoa kandarasi ya kazi hii
kwa taasisi ya World Elephant Centre ya nchini Tanzania inayotarajiwa
kuongeza hali ya usalama wa tembo hifadhini.
Teknolojia
hiii inawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua
walipo, wanapopita, kasi yao ya kutembea, sehemu wanazojificha,
wanazokunywa maji, wanazopumzika, maeneo wanayokaa kwa muda mrefu, kama
wamekufa, wamejeruhiwa,wamehama hifadhi moja hadi nyingie na taarifa
nyingine nyingi hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori
kufuatilia usalama wao.
Kola hizo zenye uwezo wa kufanya kazi kwa miaka mitatu bila kubadili betri zake zinafungwa kwa Tembo 30 wanaoongoza makundi 30.
Wataalam
wa Uhifadhi wakiongozwa na Dk. Alfred Kikoti (wa kwanza kulia)
wakiendelea na zoezi la uwekaji kola maalum kwa tembo zinazosaidia
kudhibiti mienendo ya tembo ndani na nje ya hifadhi ya Mfumo wa Ikolojia
wa Ruaha Rungwa.
Zoezi la uvalishaji wa kola maalum kwa tembo katika hifadhi ya Ruaha likiendelea.
Helikopta
maalum inayotumiwa na madaktari kwa ajili ya kutambua na kupiga dawa ya
usingizi kwa tembo kabla ya uvalishaji wa kola maalum.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (mwenye kofia) akishuhudia zoezi la
uvalishaji kola maalum kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Daktari
wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI)
akijiandaa kumdunga sindano ya kumzindua tembo baada ya kukamilika kwa
zoezi la kumvalisha kola maalum.
Picha
ya pamoja ya wahifadhi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa program maalum
ya uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari mkoani Iringa wakati wa zoezi la uvalishaji kola kwa
tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134
ARUSHA
Baruapepe: dg@tanzaniapaks.com
Wavuti: www.tanzaniaparks.com
No comments:
Post a Comment