Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye
pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay akifungua warsha ya wiki
moja ya mafunzo juu ya elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili
iliyojumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini,
waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau
mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna
ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii
inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika
wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Na Mwandishi wetu, Loliondo
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.
Hayo
yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi.
Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii
kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na
Maadili.
Warsha
hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa
dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.
Wadau hao wanatoka ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji na wilaya.
Lengo
la warsha hiyo ni kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta
mabadiliko sahihi katika jamii inayofanyika katika hoteli ya
Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani
Arusha.
Bi
Nailejileji alisema idadi ya ukeketaji Loliondo inaonyesha kupungua hadi
kufikia 57% mwaka 2015 ikilinganishwa na 87% mwaka 2014 kwa wanawake
waliojifungulia hospitalini.
Alisema
kwamba matokeo hayo yamefanikiwa kutokana na mkakati maalum unaofanyika
shuleni kwa kuanzisha vituo vya kirafiki kwa vijana vinavyolenga kutoa
elimu na hamasa kuhusu masuala ya ukeketaji.
Aidha
mafanikio hayo ni miongoni mwa jitihada za Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kueneza hamasa shirikishi katika jamii, kuelezea
ukubwa wa tatizo, athari zinazotokana na ukeketaji kwa kuwashirikisha
wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kuchukua hatua zipasazo
kukomesha ukatili huu dhidi ya wasichana.
Wazee
wa kimila wa kimasai ni watu wenye kuheshimika na kusikilizwa kwenye
jamii pale wanapotoa matamko mbalimbali yanayopelekea kuleta mabadiliko
katika jamii ambao wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa katika kukomesha
ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ambao huozwa baada ya
kufanyiwa ukeketaji mwezi Desemba kila mwaka.
Changamoto
hizo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na kile kilichoonekana na washiriki
kuwa ni mila na tamaduni zilizojengeka katika jamii ya Kimasai kwa
vijana kupokea amri kutoka kwa wazazi wao hata kama jambo hilo halina
tija katika jamii.
Wakichangia
dhana ya mtoto na kijana ni nani, majukumu yao na wana haki gani katika
jamii, wadau hao wa jamii ya kimasai walisema kuwa mtoto ni kati ya
umri 0-18 na kijana ni yule anayeanzia miaka 18-35.
Wakizungumzia
kuhusu haki walisema kwamba mtoto ana haki za kupata huduma muhimu kama
kupata elimu, kupata matunzo bora, kuishi kwa usalama au kulindwa, kuwa
na afya bora na kuheshimiwa mawazo yake.
Lakini
, hata hivyo walisema kwamba, kutokana na tamaduni iliyojengeka
miongoni mwa vijana kujifunza na kuiga malezi kutoka kwa wazazi wao,
imekuwa ni changamoto kubwa kuhamasisha vizazi kupiga vita mila na
desturi zinazoathiri wanawake.
Afisa
Elimu ya Afya na Ukimwi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Mathias Herman akizungumza kwenye warsha ya wiki moja ya
mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga
wa jadi, waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na
wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika
ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi
shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli
ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani
Arusha.
Hata
hivyo walisema pamoja na kwamba mabadiliko huchukua muda mrefu, lakini
yanaweza kufanikiwa ikiwa wanawake wa kimasai wenyewe watayavalia njuga
masuala yanayowahusu katika jamii na yanayohatarisha maisha yao.
“Ndio
mila na tamaduni zipo na kuna msemo unaosema kwamba mkataa kwao ni
mtumwa, lakini zipo tamaduni ambazo ni hatarishi na anayeathirika kwa
kiasi kikubwa ni wanawake na wasichana,”alisema Nailejileji Joseph.
Mazingira
waliyokulia Wanawake wa jamii ya Kimasai yamejenga ukimya miongoni mwao
na kuona kwamba changamoto zozote zinazotokea ni jambo la kawaida na
hazizungumziki.
Kwa
mfano ndoa za utotoni kwa wasichana wa Kimasai ni mwendelezo wa
tamaduni hatarishi unaotokana na majukumu ya mtoto au kijana katika
jamii ya kupokea anachoamrishwa na wazazi bila kuelewa athari zinazoweza
kumpata mtoto wa kike wa jamii hiyo.
“Mimi
nalea mjukuu na binti yangu yaani mama wa huyu mjukuu. Binti yangu
amepata ulemavu wa maisha baada ya kujifungua huyu mtoto akiwa na umri
wa miaka 13,”alisema Bi. Noorkidemi Kitupei mkazi wa kijiji cha
Ilopolum, tarafa ya Loliondo. Binti huyu (jina linahifadhiwa) ni mke wa
tatu kuolewa na mume wake akiwa katika umri mdogo baada ya baba yake
kuamrisha aolewe.
Changamoto
nyingine kama hiyo ilimpata binti mmoja wa kimasai aliyeolewa akiwa na
umri wa miaka 13 baada ya kupigwa na kuumizwa mkono na kuachiwa kovu
kubwa sana na mumewe baada ya Ngómbe mmoja wa mume wake kupotea, mume
wake alichukua jukumu la kumpiga karibia kumpa ulemavu wa mkono baada ya
kumuuliza binti huyo kwanini Ngómbe huyo amepotea na kujibiwa kwamba
alikuwa amelala.
Kwa
mujibu wa Mratibu huyo wa afya ya uzazi visa kama hivyo vinaendelezwa
kwa sababu hamasa bado ni ndogo katika jamii ya kimasai na wadau
wachache wanaobahatika kupata mafunzo au kwa woga unaotokana na
muendelezo wa tamaduni hatarishi zimekuwa hazihamasishwi na haziwafikii
walengwa.
Inategemewa
kwamba kituo cha redio cha jamii Loliondo FM kitatoa mchango mkubwa wa
kuhamasisha jamii masuala mbalimbali ya kijamii na kimaendeleo.
Mtaalamu
wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (katikati)
akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia
Irafay (kulia) wakati warsha hiyo ikiendelea. Kushoto ni Afisa wa
UNESCO, Hamidun Kweka.
Pichani
ni mjumuiko wa wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa
dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii wanaohudhuria
warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro.
Afisa
Elimu ya Afya na Ukimwi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Mathias Herman (wa pili kushoto) akiendesha mafunzo ya uelewa
juu ya dhana ya Utamaduni kwa mifano hai katika warsha hiyo ya wiki
inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika
wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Mshiriki ambaye ni
mkalimani wa lugha ya kimasai, Joseph Ndaika na kulia ni wanawake wa
kimasai wanaoshiriki warsha hiyo.
Mtaalamu
wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (kulia)
akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa kuhakiki kazi za vikundi katika
warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye kazi za vikundi.
Mwandishi wa Habari kutoka Redio Jamii ya Loliondo FM, Merry Jacob akiwasilisha kazi ya kikundi chake.
Kaimu
Sheikh wa wilaya ya Ngorongoro na Sheikh wa kata ya Lolieni, Khamis
Athumani akitoa mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment