Katibu
wa soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala, John Nombo
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es
Salaam leo asubuhi, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa
mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko sita ya Manispaa hiyo.
Kulia ni Mwezeshaji wa Sheria wa Soko hilo, Aisha Juma na Saada Ngunde.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Saada Ngande akizungumza katika mkutano huo.
Mwezeshaji
wa Sheria, Irene Daniel (kushoto), akizungumza kuhusu kazi alizofanya
za kusaidia watu kujua haki zao. Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa
Wanawake katika Soko hilo, Happyness Urono.
Mwenyekiti
mstaafu wa Umoja wa Wanawake katika Soko hilo, Happyness Urono,
akizungumzia changamoto walizokuwa nazo katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria, Irene Daniel akionesha mabango yanayohamasisha masuala ya haki ya mwanamke katika soko hilo.
Na Dotto Mwaibale.
UJASIRI
wa Wawezeshaji Sheria wanawake katika soko la Tabata Muslim lililopo
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam umesaidia kupunguza vitendo vya
ukatili wa jinsia katika soko hilo.
Hayo
yalielezwa na Mwezeshaji wa sheria katika soko hilo, Irene Daniel
wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi
ambao wapo katika ziara ya kutembelea masoko ya manispaa hiyo kuona
jinsi vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyopungua baada ya Shirika la
Equality for Growth kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko
hayo.
"Ujasiri
tuliofundishwa sisi wawezeshaji wa sheria katika masoko na EfG wa
kufuatilia matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia umesaidia sana
kupunguza vitendo hivyo katika soko letu" alisema Daniel.
Akitolea
mfano alisema mbali na kufuatilia masuala hayo ya ukatili katika soko
hilo pia aliweza kuisaidia familia moja baada ya baba wa familia hiyo
kutaka kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mke wake ambapo alikwenda
kuzungumza na baba huyo ambaye alikubali kubadilika.
Alisema
baba huyo ambaye alikuwa anashinda vijiweni baada ya kujitambua
alimpatia mtaji wa fedha ambapo alianzisha biashara ya maji na sasa
msuguano na mke wake umekwisha na wamefikia hatua ya kuwa na eneo lao la
biashara ya mama lishe na uuzaji wa maji.
Katibu
wa soko hilo John Nombo alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo katika
soko hilo ni lugha za matusi, wateja kuvaa nguo fupi zilizokuwa
zikionesha miili yao hivyo kuwafanya vijana kuwa na matamanio na kuanza
kuwatomasa lakini hivi sasa vitendo hivyo havipo tena.
Mwezeshaji
wa sheria Saada Juma alilalamikia jeshi la polisi kituo cha Tabata
kushindwa kushughulikia kesi ya mdogo wake aliye dhalilishwa na kijana
mmoja katika soko hilo ambapo licha ya kijana huyo kufahamika alipo
lakini polisi wameshindwa kumtia nguvuni.
Mwenyekiti
mstaafu wa Umoja wa Wanawake katika soko hilo, Happyness Urono alisema
vitendo vya udhalilishaji katika soko hilo hakuna kwani mafunzo
waliopatiwa na EfG yamewafanya wajitambue na kuzijua haki zao ambapo
ametoa mwito kwa wanawake kuzidisha umoja wao katika kila jambo.
No comments:
Post a Comment