Ikiwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bado ina mtihani mgumu wa kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Algeria baada ya mchezo wa waliocheza uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kukubali kutoa sare ya goli 2-2, kwa upande wa majirani zao timu ya taifa ya Uganda imeendeleza ubabe dhidi ya Togo.
Uganda ambao walikuwa na nafasi nzuri baada ya kuifunga Togo goli 1-0 ugenini iliendeleza ubabe wake mbele ya Togo kwa mara ya pili mfululizo, mchezo wa pili uliochezwa leo November 15 Uganda wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 hivyo Togo imeaga rasmi harakati za kuendelea kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi.
Kwa upande wa Uganda bado Farouk Miya aliendelea kuwa mwiba mkali kwa Togo baada ya kuwafunga tena katika mchezo wa marudiano Farouk Miya alifunga goli mbili dakika ya 41 na 45 baada ya Geoffrey Massa kuifungia Uganda goli la kwanza dakika ya 4 ya mchezo, ila mchezo wa November 15 Hamisi Kiiza wa Simba alikuwa benchi kwa dakika zote 90 pamoja na beki wa Yanga anayeichezea Togo Vincent Bossou huku Juuko Murshid wa Simba akicheza kwa dakika zote 90.
Video ya magoli ya Uganda Vs Togo
Matokeo ya mechi nyingine iliyochezwa na kumalizika November 15
-
Zambia 2 – 0 Sudan
No comments:
Post a Comment