Tume
ya taifa ya uchaguzi imeombwa kuweka wazi mapema iwezekanavyo tarehe ya
kupiga kura ya ubunge jimbo la Lulindi vinginevyo ucheleweshaji huo
unaathari kwa wapiga kura na vyama vyenye wagombea.
Tume ya taifa ya uchaguzi ililazimika kusitisha upigaji kura ya
ubunge katika jimbo la Lulindi baada ya jina la mgombea wa chama cha
wananchi CUF Amina Thomas Msham kukosewa katika karatasi za kupigiwa
kura na kusomeka Msham Thomas Mcham.
Akizungumzia hilo mdhamini wa chama cha NLD ambaye pia ni mgombea
wa jimbo la Lulindi Modesta Makaidi na uongozi wa chama cha mapinduzi
mkoa wa Mtwara wameonyesha wasiwasi wao na kuzungumza haya.
Akizungumza kwa njia ya simu msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo
Beatres Maiko amesema analitambua hilo na kwa sasa yuko jijini Dar es
Salaam kufuatilia suala hilo.
Jimbo la Lulindi limefanikiwa kufanya uchaguzi wa rais na madiwani,
wagombea ubunge wanaotarajiwa kupigiwa kura ni Jerome Bwanausi wa CCM,
Modesta Makaidi wa NLD na Amina Thomas Msham wa CUF, jimbo lingine
linalotarajiwa kufanyiwa uchaguzi mkoani Mtwara ni la Masasi mjini
kutokana na mgombea wake Emmanuel Makaidi kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment