TB Joshua Ayeyuka Ghafla...... Aacha Maswali Mazito Hapa Nchini - LEKULE

Breaking

6 Nov 2015

TB Joshua Ayeyuka Ghafla...... Aacha Maswali Mazito Hapa Nchini


Muhubiri wa kimataifa nabii maarufu duniani Temipote Balogun maarufu kama TB  Joshua ameacha maswali baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Magufuli.

TB Joshua aliwasili nchini November 03 kwa ndege binafsi na kupokewa na Dk.MAGUFULI pamoja na Mbunge mteule Mwigulu Nchemba katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere,Dar es salaam.

Baada ya kuwasili alifanya mazungumzo ya faragha na Dk.MAGUFULI pamoja na rais mstaafu Jakaya Kikwete kisha kufanya mazungumzo zaidi ya saa tatu na Edward Lowassa.

Ujio wa nabii huyo ulionekana kama amekuja kwa ajili ya kuapishwa kwa Dk.Magufuli lakini huku baadhi ya wananchi wakifurahishwa na ujio wake na kuamini ni fursa pekee ya kukutana naye na kufanya maombi akiwa hapa nchini.


Baadhi ya watu walisema waliamua kwenda uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kumuona nabii huyo lakini haikuwa hivyo na hawakufahamu kwa nini hakuhudhuria sherehe hizo.

No comments: