10 Nov 2015

Siku ya pili baada ya Dk.MAGUFULI kutembelea Muhimbili..ukweli wa mashine za CT Scan ni huu

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Hussein Kidantu na kumteua Prof. Lawrence Mseru kushika nafasi hiyo.
Kati ya maagizo Rais aliyoacha ni pamoja na mashine za CT Scan pamoja na MRIkuhakikisha zinatengenezwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema baada ya kukutana na kamati tendaji ya hospitali hiyo leo na Kaimu Mkurugenzi aliyeteuliwa Prof.Lawrence Mseru ametoa maelezo na kuhakikisha watafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Rais ndani ya muda waliopewa.
“Tayari suala la CT Scan na MRI limeanza kufanyiwa kazi na ameanza kuzungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Philips ya Uholanzi ili waweze kuanza kutengeneza mashine hizi, wameanza mazungumzo leo, kuanzia kesho tutaanza kuona mabadiliko yakifanyika, tutahakikisha suala hili linafanyiwa kazi kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma” Eligaesha
Wagonjwa wanaotumia mashine za MRI kwa siku ni wagonjwa 10 hadi 15 na kila mgonjwa hutumia zaidi ya dakika 40 kutumiwa na kipimo cha CT Scan wagonjwa wenye uhitaji ni kati ya 20 hadi 25..“Wagonjwa wamekuwa wakipata taabu sana baada ya mashine hizi kuharibika na imewabidi kwenda hospitali binafsi ili kuweza kupata vipimo ambavyo huku ni gharama zaidi ya hapa” Eligaisha.
Amesema kwa sasa wanafanya juu chini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Pia amesema Serikali ndiyo ilisaini mkataba wa kutengeneza mashine hizo na ndio sababu wameweza kulipa fedha kwa ajili ya matengenezo hayo.

No comments:

Post a Comment