10 Nov 2015

Matatu kutoka kwa Mbunge mwenye elimu ya darasa la saba.. Uzoefu, shule? Bunge?

Kishimba
Jumanne Kishimba
 ‘Nawashukuru sana wapiga Kura wa Kahama kwa kunichagua, nilijaribu mwaka 2000 wakati Jimbo la Msalala halijagawanywa lakini tulifutwa Wagombea wote wa CCM kulikuwa na rafu kidogo tulicheza. Toka mwaka 2000 sikuwahi kugombea mpaka mwaka huu 2015‘ >>> Jumanne Kishimba, Mbunge mteule Jimbo la Kahama.
Jumanne Kishimba (wa kwanza kulia) akisaini daftari la wageni.
Jumanne Kishimba (wa kwanza kulia) akisaini daftari la wageni.
Jumanne Kishimba aliwahi kuendelea kuiwaza Siasa baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza? >>> ‘Imekuwa kwenye ndoto zangu kwa kuwa biashara na siasa ni kama mtu na ndugu yake, kulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa elimu yangu ni darasa la saba lakini nina uzoefu wa kutembea sehemu nyingi na nimefanya kazi nyingi, ni vizuri kukawa na mchanganyiko wa wenzetu wenye elimu na sisi wenye uzoefu tukatatua changamoto pamoja Bungeni‘. >>>
Anazijua changamoto za wananchi wake? >>> ‘Wananchi wangu wanahitaji dawa, dispensary, maji, umeme.. ni vitu ambavyo elimu ya darasa la saba kwa Mbunge sio tatizo, Bungeni huendi kufanya operation kwamba unaweza kuua watu. Bungeni ninapeleka mawazo ya walionituma na kuongeza ya kwangu kwa kuwa una uzoefu‘. >>>Jumanne Kishimba.

No comments:

Post a Comment