Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana
na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa
nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na
mashambulizi ya kigaidi majuzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na
Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu
cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois
Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya
kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi
huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi
huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi
Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.
====
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi
130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini
Paris, Ufaransa.
Pamoja na kutia
saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa
Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na
ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu
Dokta Magufuli
ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema
Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki
kigumu cha majonzi.
Aidha Rais
Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze
kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku
Katika hatua
nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli
amewasili Mjini Dodoma kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
Mheshimiwa
Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya
shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa
na;
Gerson
Msigwa
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November
17, 2015
No comments:
Post a Comment