Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
SSRA, Omar Kahlfan, (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema
Muro, (wapili kushoto), Meneja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari wa
PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, NHIF, (kulia waliosimama), wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa
PSPF, Bw. Adam Mayinhu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Michael Mhando, wakitia saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi
hizo mbili kushirikiana ambapo Wanachama wa PSPF wa Uchangiaji wa Hiari,
watadhaminiwa na Mfuko huo ili waweze kuingizwa kwenye utaratibu wa
kupatia bima za afya kutoka NHIF. Makubaliano hayo yaliyofikiwa leo
Jumatano Novemba 18, 2015 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia
makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa
Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali
zote zenye mkataba na NHIF.
Makubaliano
hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama
wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi
huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadi za
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli,
ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilizo bora.
“ Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa PSPF
kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa
huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.”
Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha, wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wapili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha, wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wapili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
Bw. Mayingu, (kushoto) na Bw. Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
Bw. Mhando hotuba yake.
Maafisa kutoka NHIF.
Mwanachama wa PSPF, akisoma vipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.
Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS.
Kaimu Murugenzi Mtendajiw a NHIF, Bw. Michael Mhando (kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro
Mwanachama
wa mpango wa Uchagiaji wa Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya,
kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan (kulia)
Mwanachama wa PSPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake
Meneja Msoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin,akitoa maelezowakati wa hafla hiyo.
Meneja
wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Penshni wa PSPF,
Bi.Mwanjaa Sembe, (wakwanza kulia), na afisa wa PSPF, wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika wakwanza wa mpango wa Mfuko huo
kuwapatia matibabu wanachma wake wa mpango wa PSS
Mzee
Mohammed Madenge, watatu kushoto), ambaye ni Mwanachama wa PSPF,
wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neon la shkrani kwa
niaba ya wenzake.
No comments:
Post a Comment