Rais John Magufuli leo amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kujionea uhalisia wa huduma inayotolewa.
Kama
ilivyokuwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha wiki
iliyopita, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa hospitali hiyo na
kuongozana nao katika maeneo ambayo aliyachagua yeye.
Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa
hususan wanaolala chini.
Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko
Tazama Video hizi kuona ilivyokuwa

No comments:
Post a Comment