Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana joto duniani.
Akizungumza
katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kiongozi huyo wa Kanisa
katoliki duniani amesema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa
kutawala ndani ya manufaa ya wote.
Kabla ya
kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili
umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati
wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.
Katika
ziara yake barani Afrika,kiongozi mkuu huyo wa kanisa katoliki
anategemea kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya
Kati novemba 30..
No comments:
Post a Comment