SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kampeni ijulikanayo
kama NSSF Kwanza ambayo itafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania,
Kampeni hiyo imeanza kwa kuwafikia wakulima kwenye vijiji vyao na
Mashamba yao Mkoani Mbeya ili kuweza kuwapa elimu juu ya hifadhi ya jamii na faida zake.
Kampeni
hiyo imeanzia kwenye Kijiji cha Iyumpi wilayani Mbozi ambako wakulima
wa Kahawa zaidi ya 44 wamejiunga na NSSF. Pia Kampeni hiyo inatarajia
kwenda Wilayani Ileje, Vijiji vya Mloo na Igamba.
NSSF
inaendelea kuwasihi Wakazi wa Mbeya na Vitongoji vyake waendelee
kujiunga na NSSF ili waweze kujipatia Mafao bora yakiwemo Bima ya
Matibabu bure kwa Mwanachama na familia yake.
Wakazi
wa Kijiji cha Itumpi wilaya ya Mbozi wakiwa wamekusanyika ili
kusikiliza elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kupitia Mpango maalumu
wa Wakulima Scheme kwenye kampeni inayoendeshwa na NSSF ijulikanayo
kama NSSF Kwanza.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro akitoa elimu kwa wakazi wa
kijiji cha Itumpi Wilaya ya Mbozi juu ya mpango wa Wakulima Scheme .
Wakulima
wa Kijiji cha Iyumpi wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na
wafanyakazi wa NSSF juu ya huduma zitolewazo na NSSF .
Maafisa
Matekelezo Mkoa wa Mbeya wakitoa elimu jinsi ya kujaza fomu ya
kujiunga na NSSF kwa mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Iyumpi.
Gari
maalumu la matangazo la NSSF likiwa limefungwa mitambo ya matangazo
ambalo hutumika kuzunguka mitaani na kutoa matangazo kwa wakazi wa
vijiji mbalimbali vya mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment