SHIRIKA la Taifa la Hifadhi yaJamii(NSSF) limetoa Elimu kwa Wenyeviti na Makatibu wa Wakulima wa Korosho na Ufuta wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi kuhusu mpango wa Hifadhi ya Jamii
kwa Wakulima, Mpango huo unamwezesha mkulima kupata mikopo mbalimbali
ikiwemo mkopo wa vifaa vya kilimo pamoja na pembejeo za kilimo.
Aidha
mpango huo unamwezesha mkulima na familia yake kufaidika na mafao
mbalimbali yatolewayo na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu ambapo mkulima
atapata matibabu bure yeye na familia yake.
Wanyeviti
na Makatibu hao waliweza kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina
kuhusu Mpango huu kwa Wakulima na jinsi ya kuwasaidia Wakulima
kuondodokana na gharama za matibabu kupitia mafao ya matibabu yatolewayona na NSSF.
Wakulima wa Korosho wa Kilwa Masoko wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa Semina.
Afisa
Ushirika wa Vyama vya Wakulima (AMCOS) Bwana Vincent Mhengilolo
akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Ushirika wakati wa
Semina iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF)
Mkulima
wa Korosho wa Kilwa Masoko akiuliza swali ili kupata ufafanuzi kuhusu
Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima Mjini Kilwa Masoko.
Afisa
Mafao wa Shirika la Taifa la Hfadhi ya Jamii NSSF Bi Lydia Ignas akitoa
ufafanuzi kuhuhu mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Lindi Bi Nour Azin akizungumza na Wenyeviti na Makatibu
wa Vyama vya Wakulima kuhusu mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima
katika semina iliyofanyika Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
Ofisa
Mafao wa NSSF, Kabonwa Kandoro akiwaandikisha uanachama Wenyeviti na
Makatibu wa vyama vya wakulima AMCOS baada ya semina iliyofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment