Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26, 2015 Jijini
Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mauzo ya nyumba
katika mradi mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam
(kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Hamad Abdallah.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya ramani ya mradi wa nyumba
ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakitembelea katika eneo la ujenzi huo.
Ujenzi ukiendelea
Waandshi
wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi huo.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
Na Philemon Solomon Fullshangweblog
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa
kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya
kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 ambao
unatarajiwa kugarimu kiasi cha zaidi ya Sh 187, 927, 105,500 mpaka
utakapomalizika .
Pia
ikumbukwe kuwa mradi huu ni seemu ya mji mpya wa kisasa (Satellite City)
unajengwa hapa ,mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es
Salaam ambalo liko mita chache kutoka fuko za bahari ya Hindi pia karibu
na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na
Mikocheni mradi huu una jumla ya nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye
majengo nane tofauti ya ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote
muhimu za kijamii.pia kutakuwepo na seemu ya maduka makubwa kwa ajili ya
wakazi na maeneo ya jirani”Alisema Mchechu.
No comments:
Post a Comment