Mtu
ambaye hajafahamika jina wala makazi, amefariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika Kituo cha Afya Katoro wilayani Geita, baada ya
kufikishwa na polisi akiwa hajitambui.
Mtu
huyo anasadikika kupigwa na watu wasiojulikana Jumamosi saa mbili
usiku, huku tukio hilo likihusishwa na chuki za kisiasa zinazohusiana na
vurugu zilizosababisha kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Geita, Alphonce Mawazo.
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Daniel Izengo alisema
saa 2:30 usiku walimpokea mtu huyo aliyefikishwa na polisi akiwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani.
Awali,
mganga huyo alisema watu wawili walijeruhiwa katika vurugu
zilizosababisha kifo cha Mawazo ambao walifikishwa kwenye kituo hicho
wakatibiwa na kuruhusiwa.
Pia
alisema watu watatu walifikishwa kituoni hapo juzi akiwamo Mawazo,
Elizabeth Paschal (48) na Bahati Michael (38) wote wakiwa wakazi wa
Katoro.
Dk Izengo alisema hali ya Mawazo ilibadilika na
kumwandikia
rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Geita ambako alifariki dunia, huku
majeruhi wengine wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa baada ya hali zao
kuridhisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Lotson Mponjoli alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea, ikiwamo kuwatafuta watuhumiwa.
Hilo ni tukio la pili ndani ya siku chache, la kwanza likiwa la kifo cha Mawazo.
No comments:
Post a Comment