Hii stori ilipewa uzito wa aina yake,
kulikuwa na upande mzuri na upande mwingine haukuwa mzuri… najua kama
uliifatilia kwa ukaribu utagundua kwamba kulikuwa na headlines
zikihusishwa na kukamatwa kwake na ishu ya udini..
Lakini kwenye upande mzuri ilikuwa dunia kuutambua na kuuheshimu ubunifu wake, akapokea pongezi nyingi ikiwemo kutoka kwa Rais Obama na Mark Zuckerberg… sio kila mtu anaweza kubuni saa kama aliyobuni Ahmed Mohamed, kijana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Texas Marekani.
Familia haijaridhika, wamerudi Mahakamani na kudai fidia ya dola Milioni 15
kutokana na kitendo cha mtoto wao kukamatwa kimakosa akihisiwa kuwa na
bomu wakati ilikuwa ni saa ambayo aliibuni mwenyewe na akaenda nayo
shule… kingine ambacho familia inalalamika ni ishu ya Ahmed kukamatwa na kuhojiwa na Polisi bila wazazi wake kutaarifiwa.
No comments:
Post a Comment