Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya
Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa
Septemba 2015.
Mshindi
wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussen Tshabalala ambapo alipigiwa
kura nyingi na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa
ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba
News.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi,
wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji
katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la
busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji
wake bora.
Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.

jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG
Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba,
Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo
ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la
mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao
wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga
kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’
Simba
News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari
mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya
wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya
Simba.
Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
No comments:
Post a Comment