Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha
mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi
Msaidizi – Shughuli za Bunge, (Pichani) kilichotokea ghafla mapema
Ijumaa ya Novemba 27.2015, wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
kwa matibabu.
Msiba
upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini Dodoma. Taarifa zaidi na
taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya maziko zitaendelea
kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu
pindi mipango itakapokamilika.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINI!
BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015.
No comments:
Post a Comment