Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.
Majipu (mambo matano) hayo ni;
1.Kudhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
2.Kukomesha rushwa na ufisadi.
3.Kufumua mtandao wa majangili.
4.Kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na
5.Kuua ‘mchwa’ unaoitafuna fedha za Serikali.

Maoni
yaliyotolewa na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida yanaonyesha
kwamba kufanikiwa kwake kutategemea aina ya ushirikiano atakaoupata
kutoka kwa wananchi na wanasiasa na hasa wa kutoka chama chake.
Mhadhiri
kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Elijah Kondi alisema Dk Magufuli anahitaji kupigana vita kali
kufanikisha ahadi zake na akaonya kuwa hawezi kusimama mwenyewe na
kushinda vita hiyo bila kuungwa mkono na wananchi hasa chama chake, CCM.
“Vigogo
wengi ndani ya chama chake wamekuwa wakihusishwa na majipu hayo. Hivyo,
kufanikisha azma hiyo, kutategemea wingi wa wanaCCM watakaomuunga
mkono, lakini kama watakuwa wachache, itakuwa vigumu. Hilo hata yeye
(Magufuli) analifahamu ndiyo maana anasema vita hiyo ni kubwa,” alisema Kondi.
Pia,
alisema kushughulikia mtandao wa dawa za kulevya, ujangili na kuanzisha
mahakama ya mafisadi kutategemea ushirikiano atakaoupata kutoka kwa
watendaji na baraza lake la mawaziri.
Kondi
alisema kushindwa kwa Rais mstaafu Kikwete katika mambo hayo kulitokana
na udhaifu wa baraza lake la mawaziri na watendaji wa taasisi za
Serikali.
“Rais anaweza kuwa na dhamira njema, lakini je, atapata mawaziri wazuri wa kumsaidia? Hao mawaziri watakuwa na ari gani ya kushiriki vita hiyo?” alihoji na kuongeza:
“Rais anaweza kuwa na dhamira njema, lakini je, atapata mawaziri wazuri wa kumsaidia? Hao mawaziri watakuwa na ari gani ya kushiriki vita hiyo?” alihoji na kuongeza:
“Kwa sababu anaweza kuanzisha mahakama ya mafisadi lakini ikashindwa kuonyesha uhai kama anavyotarajia.
"Jaribio la kutumbua majipu hayo itategemea ushirikiano wa chama chake, mawaziri atakaowateua na watendaji wa Serikali.”
"Jaribio la kutumbua majipu hayo itategemea ushirikiano wa chama chake, mawaziri atakaowateua na watendaji wa Serikali.”
Mhadhiri
wa Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Richard Mbunda alisema kilichosababisha marais waliomtangulia kushindwa
kutumbua majipu hayo ni utofauti mkubwa ulioonekana kati yao.
“Utofauti
katika uwezo wao ukoje? Dhamira zao zinatofautianaje? Lakini hata
kiwango cha utashi wa kushughulikia hilo jipu kinatofautianaje na
uongozi uliopita. Ukisikiliza kauli ya Rais Magufuli anaonyesha
matumaini,” alisema Mbunda.
Meneja
wa Soko la Machinga Complex, Nyamsukura Masondore alisema kupandishwa
mahakamani kwa vigogo wa Serikali katika kashfa ya EPA ni sehemu ya
juhudi zilizoonekana kwa uongozi uliopita.
“Hivyo, hakuna kitakachoshindikana kwa Rais Magufuli endapo watendaji wa chini watakuwa tayari kubadilika na kutoa ushirikiano wa kushinda vita ya majipu hayo,” anasema
“Hivyo, hakuna kitakachoshindikana kwa Rais Magufuli endapo watendaji wa chini watakuwa tayari kubadilika na kutoa ushirikiano wa kushinda vita ya majipu hayo,” anasema
Profesa
George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema ana imani Rais
Magufuli anaweza kushughulikia changamoto hizo sugu ambazo ameziita
majipu kutokana na historia ya utendaji wake.
“Rais Magufuli atafanikiwa kazi hiyo kutokana na historia yake ya kutojihusisha kwa karibu na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na nje,” alisema.
“Rais Magufuli atafanikiwa kazi hiyo kutokana na historia yake ya kutojihusisha kwa karibu na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na nje,” alisema.
Profesa
Shumbusho alisema kuwa endapo ataendelea na msimamo huo, changamoto ya
ukwepaji kodi, misamaha ya kodi, biashara haramu ikiwamo ya dawa za
kulevya zitakoma.
Dawa za kulevya
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi alinukuliwa Agosti 2013 bungeni akikiri kuwapo baadhi ya majina
ya wabunge miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya
dawa za kulevya lakini alisema Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa
haraka.
Hata
Kikwete wakati wa awamu yake ya kwanza, aliwahi kusema anawajua wauza
dawa za kulevya lakini tatizo hilo limeendelea kuwa sugu hadi anamaliza
kipindi chake cha pili.
Mwaka
huohuo, Umoja wa Mataifa (UN) ulitoa ripoti inayobainisha Tanzania kuwa
kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki.
Kuanzia 2010 hadi 2013 ilipitisha tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine na ikitaja Bandari ya Tanga kuwa njia kuu ya upitishaji huo.
Kuanzia 2010 hadi 2013 ilipitisha tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine na ikitaja Bandari ya Tanga kuwa njia kuu ya upitishaji huo.
Je,
baada ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za
Kulevya ya mwaka 2015, Rais Magufuli ataweza kusimamia mapambano dhidi
ya vinara wa biashara hiyo?
Ujangili wa tembo
Kabla
ya kuondoka madarakani, Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa Februari 2014
na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) akikiri kuwatambua
majangili 40 wa meno ya tembo na kwamba kiongozi wao anaishi Arusha.
Pia, alikiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu.
Vilevile,
Mei 2014, ripoti iliyoitwa ‘Ivory’s Curse: The Militarization and
Professionalization of Poaching in Africa’, ilieleza kuwa tangu mwaka
2000 wizara inayohusika na utalii ilikuwa imetawaliwa na kashfa za
rushwa. Ripoti hiyo ilifafanua jinsi vikundi mbalimbali vya waasi barani
Afrika vinavyoendesha shughuli za ujangili.
Katiba ya Jaji Warioba
Oktoba
2014, Bunge Maalumu la Katiba lilipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa
tofauti ya kura mbili tu zilizonusuru kukwamisha Katiba hiyo kwa upande
wa Zanzibar. Mvutano kati ya CCM na upinzani wakati wa upitishaji wa
Katiba hiyo ulitokana na tofauti za itikadi na sera kuhusu muundo wa
Muungano.
Wajumbe
wa CCM walipigania sera yao ya muungano wa Serikali mbili wakati wenzao
wa wapinzani walipigania muundo uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba chini ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba wa Serikali Tatu. Hadi
sasa haijapigiwa kura ya maoni.
‘Mchwa’ Serikalini
Kila
mwaka, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa
akikagua na kuibua ufisadi mkubwa katika Serikali Kuu, Idara za Serikali
na mashirika ya umma.
Ripoti iliyotolewa mwaka huu inaonyesha ukaguzi ulifanyika katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109.
Kikwete amewahi kupangua baraza lake la mawaziri na kuwafukuza kazi watendaji lakini bado ufisadi umeendelea katika nyanja tofauti kama ulipaji mishahara hewa na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

Mahakama ya mafisadi
Moja
ya ahadi kubwa za Rais Magufuli wakati wa kampeni na Novemba 20
alipozindua Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano ni kuanzisha
Mahakama Maalumu ya kushughulikia mafisadi.
Tayari mchakato umeanza lakini wachambuzi wanasema kinachotakiwa ni kuipa meno Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili iweze kufanya kazi zake bila kuogopa mtu.
Tayari mchakato umeanza lakini wachambuzi wanasema kinachotakiwa ni kuipa meno Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili iweze kufanya kazi zake bila kuogopa mtu.
No comments:
Post a Comment