Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue jana alifanya ziara katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni muendelezo baada ya Rais Dk. MAGUFULI
kufanya ziara ya kushtukiza.
Baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukagua
vitanda vilivyonunuliwa baada ya agizo lake, Sefue alitoa maamuzi
yaliyofikiwa…
Majibu kutoka Ikulu kuhusu mashine za CT Scan na MRI
“Nimekagua mashine hizi za kukagua magonjwa MRI na CT Scan, chanzo cha
kuharibika tena ni kukaa muda mrefu bila kutumika,sasa hivi spea zote
zimefika, kazi ya kutengeneza inaendelea, MRI nimehakikishiwa ndani ya
siku tatu itakuwa inafanya kazi, kuhusu CT Scan nimeambia kesho(leo) inaweza
kuanza kufanya kazi”..
“Lazima mafundi kutoka Philips
wakae muda wa wiki moja baada ya kutengenezwa kujiridhisha
zimekamilika..bado tuna mpango wa kuongeza mashine hizi ili angalau tume
na mbili mbili..,kuhusu madeni ya mshine hizo..
"Ni kweli kulikuwa na
madeni lakini tumeanza kuyalipa kwa sasa suala hilo halipo tena,
tulikuwa tunadaiwa na Philips bilioni 7 na Serikali tayari ililipa
bilioni 3 nyingine zinapaswa kulipwa na waliokuwa wakipata huduma ya
mashine hizo“… Ombeni Sefue.
Maduka ya Bohari ya dawa MSD kujengwa ndani ya hospitali kubwa..“Tuna
tatizo la kibajeti, tunahitaji bajeti ya kama bilioni 248, bajeti
unakuta inafikia kama bilioni 70, hili inabidi tushughulike nazo hasa
katika hospitali kubwa pamoja na zile za rufaa, MSD wanapaswa kufungua
maduka yao ndani ya hospitali..na lazima kuwa na dawa zote, hospitali ya
Muhimbili duka la madawa litafunguliwa rasmi Jumatatu”..Ombeni Sefue.
Ishu ya wizi wa dawa za Serikali pia imesikika...“Tutumie
mifumo ya TEHAMA kuhakikisha hakuna dawa ya Serikali inaibiwa, pia
tujue kwamba kila dawa inatumiwaje na daktari, ufumbuzi wa matatizo haya
upo, kwa wale wa maduka ya dawa binafasi ambao wanajijua wanatumia dawa
za serikali michezo hiyo, basi, dawa zetu tutakuwa tunaziwekea nembo,
ukigundulika ujue mwisho wako basi, mnapaswa kutambua dawa hizi
zinanunuliwa na kodi ya wananchi hivyo tutadhibiti tabia hii” ...Ombeni Sefue.
Huduma mbaya kwa wagonjwa “Tutoe
huduma nzuri kwa wananchi, tuwahudumie kwa upendo na wakati, kuanzia
sasa kila mtumishi wa umma lazima avae jina lake ili anayemuhdumia ajue
anahudumiwa na nani, nitaanza na mimi..ili ikitokea malalamiko ajue
anaanzia wapi, na lazima kila ofisi iwe na dawati la msaada ili kila
mwananchi aweze kupiga simu na kuweza kutatuliwa tatizo lake”…Ombeni Sefue.
Kuhusu safari za nje kwa viongozi...“Tumetumia
fedha nyingi sana kwenda nje, nyingine za lazima na nyingine sio za
lazima, mfano mafunzo sasa ni mwisho, tunavyo vyuo vingi vyenye uwezo wa
kutoa mafunzo badala ya kwenda nje ama ni rahisi kuleta mtaalam hapa
kuliko kupeleka watu 10 kwenda kwenye mafunzo..
"Sasa hivi itakua mbinde
mtu kuweza kusafiri..si kwamba hatutahudhuria mikutano lakini Rais
amesema mabalozi wetu watatumika pale inapobidi”...Ombeni Sefue.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia), akisikiliza
maelezo kutoka kwa mtaalam wa Mashine ya CT-Scan katika hospitali hiyo.
23 Novemba, 2015
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (mwenye suti ya kijivu),
akimsikiliza mmoja wa Wagonjwa aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya
Mifupa (MOI), ambayo ilipata vifaa mbalimbali kutokana na agizo la Mhe.
Rais la kuboresha huduma katika Taasisi hiyo. 23 Novemba, 2015
Pichani; Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo inafanyiwa matengenezo. 23
Novemba, 2015
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa tatu kulia), akitoa
maelezo kuhusiana na ziara yake hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa
habari. 23 Novemba, 2015
No comments:
Post a Comment