Uchapakazi
wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa Tanzania
pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi hizo
kwenye wakati mgumu.
Kenya
ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni,
imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama
yeye.
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
Ziara
yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu mwingi
na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo na
kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.
Ili
kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya kugharamia
safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua kuzisitisha mara
moja.
Dkt
Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225 zilichangwa
kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini Dodoma
zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15 pekee
zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo.
Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili.
Jumatatu
hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru
December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo mengine
muhimu.
Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya.
Hizi ni baadhi ya tweets za wakenya:
No comments:
Post a Comment