Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti
linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers (TSN)
mapema jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia
utendaji wa kazi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel (wa kwanza kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi
katika minara ya shirika hilo Kisarawe.
Profesa
Elisante amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo
ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Tanzania Standard
Newspapers (TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lengo likiwa ni
kufahamiana na wafanyakazi, kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua
changamoto zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU
ya awamu ya Tano. Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.
Clement Mshana.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel akiangalia tofauti ya santuri ya zamani na flashi ya kisasa
zinavyozidiana ukubwa kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika
ofisi za shirika la utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea
na menejimenti ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika
kipinda shirika hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam.(RTD).
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za
kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati
alipotembelea shirika hilo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona
utendaji wake.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(wa pili kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza
kutengeneza batiki na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la
Sanaa Tanzania(BASATA) mapema jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment