Kampuni ya TTCL Yakisaidia Vifaa Tiba Kituo cha Afya Buguruni Dar - LEKULE

Breaking

19 Nov 2015

Kampuni ya TTCL Yakisaidia Vifaa Tiba Kituo cha Afya Buguruni Dar

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa tatu kushoto)  akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada katika kituo cha afya cha Buguruni leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea na kushoto kwake ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
KAMPUNI  ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imekitembelea kituo cha Afya cha Buguruni cha jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa pamoja na dawa kwa ajili ya kukiwezesha kutimiza majukumu yake ya kuwahudumiwa wagonjwa mbalimbali wanaokitegemea kituo hicho.



Katika zoezi hilo, TTCL imekabidhi mashuka 100, Vyandarua 100, Maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho kwa ajili ya kuwahudumiwa wakazi wa maeneo hayo kiafya.




Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemas Mushi alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa kampuni hiyo katika kurejesha faida kwa wananchi ambao ni wateja wa kampuni hiyo. Alisema wanaamini msaada huo unaenda kuwahudumia wananchi ambao ndiyo wateja wa kuu wa huduma za TTCL.




"...Vifaa hivi vinakwenda kuwatibu wananchi ambao tunaamini ni wateja wetu, hivyo wakiwa na afya njema ndiyo furaha kwetu na kuendelea kushirikiana nao kihuduma. Huu ni utaratibu wetu wa kawaida kila tunapopata kidogo tunakirudisha kwa wananchi...leo tumetoa mashine, mashuka 100, vyandarua 100 na dawa ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwa wateja wetu," alisema Meneja huyo wa TTCL.



Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Maofisa Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Buguruni (kushoto) akimshukuru Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada huo ambao ni pamoja na vifaa tiba.
Alisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na kituo hicho cha afya na hasa kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao umekuwa changamoto kwa jiji la Dar es Salaam. 



Kwa upande wake, Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea ameishukuru kampuni ya simu Tanzania kwa ukarimu wao na kuamua kukisaidia kituo hicho kwani wamesaidia kutatua changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho katika kutoa huduma za afya. Aliomba makampuni mengine kufuata nyayo za TTCL kusaidia kutatua changamoto za huduma za afya katika vituo vya afya na hospitali anuai kulingana na mahitaji ya maeneo husika.




Kituo cha afya cha Buguruni ambacho leo kimenufaika na msaada huo ndicho kilichoteuliwa katika eneo hilo kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao ulilipuka hivi karibuni kwa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam na ambapo madhara yake yaliziathiri baadhi ya jamii jijini hapa.

No comments: