Afisa
Maendeleo ya Jamii (W) Ngorongoro, Teresia Irafay (wa pili kushoto)
akiitambulisha meza kuu kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Wilaya ya
Ngorongoro, Lemuel Kileo, (wa tatu kulia) kufungua kongamano la
viongozi wa mila wa kabila la wamasai (Laigwanan/Ngaigwanani) na
wanawake Mashuhuri yenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu
zinazorudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji. Kushoto
ni Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi
kutoka (UNESCO), Bi. Rose Haji Mwalimu, Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya
Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu (wa pili kulia) pamoja na Katibu wa Baraza
Mila (W) Ngorongoro, Laanoi Munge, (kulia), Mwenyekiti wa Baraza la
Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai (wa tatu kushoto).
JAMII
ya wafugaji imetakiwa kutumia juhudi zao binafsi kubadilisha mawazo na
imani ya jamii kwamba mila na desturi hazibadiliki ili kutengeneza mfumo
bora mpya unaothamini maisha ya wanawake.
Wito
huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii
na Mkufunzi, Bi. Rose Haji Mwalimu wakati akiwasilisha mada kwenye
kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai
(Laigwanan/Ngaigwanan), Laiboni na wanawake Mashuhuri yenye lengo la
kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo katika
jamii za wafugaji.
Aliwataka
washiriki wa warsha kusimama kidete na kutumia elimu waliyoipata katika
kushawishi jamii kubadilika na kuachana na mila za ukekeketaji,ndoa za
utotoni na pia unyanyasaji mwingine wa kijinsia unaoonesha ubabe wa
wanaume na mfumo dume.
Aliwataka
wanajamii hao kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari,
rediojamii, vikao mbalimbali vya kata na vijiji pamoja na nyumba za
ibada kuhimiza watu kubadilika na kuacha mila hizo za ukeketaji na
kuozesha watoto katika umri mdogo.
Aidha
Bi. Rose Haji Mwalimu katika kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, (UNESCO) amewataka
wanawake kuvunja ukimya na kuacha uoga na kuibua vitu vinavyowanyima
haki zao za msingi.
KatibuTawala
wa Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kileo akifungua kongamano la viongozi
wa mila (Laigwanan/Ngaigwanan na Laibon) pamoja wanawake mashuhuri lenye
lengo la kuondoa mila potofu zinazokwamisha maendeleo katika jamii za
wafugaji ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro.
Aliwataka
wanawake kujitambua ili kutumia sheria zinazowalinda kuondokana na
unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia unaoendelea katika jamii za
kifugaji na kuwaomba viongozi wa mila washiriki katika kuondoa mfumo
dume.
Naye
Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Benezeth
Bwikizo, amesema kama watuw atajitokeza na kueleza ukweli serikali
itachukua hatua hasa ya kulinda wanawake na watoto kupitia mamlaka
iliyokabidhiwa na Katiba ya nchi.
Alisema
kwa mujibu wa sheria Serikali ina mamlaka ya kuhakikisha kwamba haki za
watoto zinalindwa kupitia sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba mtoto lazima alindwe na apate
haki zake zote za msingi.
Alisema
pamoja na katika na sheria zilizotungwa, mtoto pia analindwa na mkataba
wa kimataifa wa haki za mtoto wa Novemba 20, 1989 inayotoa ufafanuzi
wa kulinda na kuhakikisha kwamba haki za mtoto zinalindwa na
kuheshimiwa.
Aliongeza
kuwa pia ulindaji huo wa haki za mtoto unakwenda sanjari na mkataba wa
Umoja wa nchi za Afrika ya mwaka 1990 unaotoa ufafanuzi juu ya haki za
msingi za mtoto na namna inavyotakiwa kuheshimiwa na kulindwa bila
kuathiri haki zao.
Ofisa Elimu ya Uzazi na UKIMWI kutoka UNESCO, Mathias Herman akizungumzia malengo ya kongamano hilo kwa washiriki.
Bw.Bwikizo,
alitaja haki za muhimu kwa mtoto zinazotakiwa kulindwa na kuheshimiwa
ili kuhakikisha mtoto anakua katika malezi bora ni huduma za afya,
chanjo, matibabu, Lishe na malezi bora kupata haki ya kuishi, haki ya
kuendelezwa na haki ya kulindwa.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kongamano hilo, KatibuTawala wa Wilaya ya
Ngorongoro, Lemuel Kileo, amelishukuru Shirika la UNESCO kwa kuendesha
mafunzo hayo ya kutoa elimu na kujenga uwezo kwa viongozi wa mila na
wanawake mashuhuri ili kuondoa mila potofu katika jamii ikiwemo
Ukeketaji, mimba za Utotoni na ndoa za umri mdogo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Bw. Kileo aliwataka viongozi na washiriki
wa warsha hiyo watumie nafasi hiyo waliyoipata kwenda kufikisha ujumbe
kwa jamii ili kupeleka maendeleo mbele kwa kupunguza vifo vya akinamama
na wasichana wenye umri mdogo, kuondokana na ukeketaji pamoja na mimba
za umri mdogo.
Mtaalamu
wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii na Mkufunzi kutoka UNESCO,
Bi. Rose Haji Mwalimu akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano.
Kwa
upande wa mmoja wa wakufunzi wa warsha hiyo kutoka UNESCO akizungumzia
malengo ya warsha hiyo, Ofisa Elimu ya Uzazi na Ukimwi wa shirika hilo,
Mathias Herman, amesema warsha hiyo ni mwendelezo wa warsha zinazotolewa
na UNESCO kwa ajili ya kutoa elimu ya kuwajengea uwezo na kugawa
majukumu kwa viongozi wa kimila (Laigwanan), wa mama mashuhuri, viongozi
wadini, wakunga wa jadi pamoja na waandishi wa habari kufanya
ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto.
Aliongeza
kuwa UNESCO inatarajia mafunzo hayo kutaleta mabadiliko kupitia nafasi
ya viongozi hao mashuhuri katika jamii kwa kuwa wanaaminika ili
kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wanaotoa mafunzo kuhakikisha
kwamba suala la mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji
linafika mwisho katika jamiii ya kifugaji.
Mwenyekiti
wa Baraza la Malaigwanan wilaya ya Ngorongoro, Joseph Oletiripai
akisisitiza jambo kwa Malaigwanan pamoja na wakina mama mashuhuri ambapo
aliwataka watumie nafasi waliyopewa na jamii na fursa ya elimu
waliyopata kutoka kwa wadau wa maendeleo UNESCO kuwa italeta mabadiliko
na mpango chanya katika jamii ya Kimasai.
Ofisa
Ustawi wa Jamii wa wilaya ya Ngorongoro, Benezeth Bwikizo (kuhoto)
akizungumzia haki za watoto. Kulia ni Mkalimani wa lugha ya Kimasaai
Mchungaji Mark Murenga.
Mama Mashuhuri kutoka kijiji cha Olopiri, Nolarir Pashuku, akitoa maoni yake kwenye kongamano.
Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo ambaye ni Laigwanan , John Olekulinja kutoka kata ya Malambo akizungumzia mafunzo hayo.
Kiongozi wa Malaiboni wilaya ya Ngorongoro Bw. Sangau Naimodu (katikati) akieleza namna inavyofaa kueneza elimu ya mabadiliko.
Mratibu
wa Afya ya Uzazi na Mtoto, tarafa ya Loliondo (W) Ngorongoro, Bi.
Nailejileji Joseph akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa washiriki wa
kongamano hilo.
Pichani
juu na chini ni viongozi wa mila wa kabila la wamasai
(Laigwanan/Ngaigwanan), Laiboni na wanawake Mashuhuri walioshiriki
kwenye kongamano hilo yenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu
zinazorudisha nyuma maendeleo katika jamii za wafugaji lilioandaliwa na
Shirika la UNESCO.
No comments:
Post a Comment